Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beiranvand; Kutoka kijana maskini asiye na makazi Tehran hadi kipa wa dunia

Muktasari:

  • Alireza anayecheza Tractor SC ya Iran,  ni mmoja wa makipa bora zaidi na wenye historia nyingi za kuvutia sana na zenye funzo maishani akitokea kwenye familia ya umasikini hadi kuibuka kipa wa dunia kwa sasa.

CALIFORNIA, MAREKANI: KIWANGO cha kipa wa timu ya taifa ya Iran, Alireza Beiranvand kimeendelea kushangaza wadau wa soka hasa baada ya kuokoa michomo mingi ya hatari katika mechi ya pili ya kundi G katika Fainali za Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Ubelgiji, iliyoisha kwa timu hizo kutoka 0-0.

Alireza anayecheza Tractor SC ya Iran,  ni mmoja wa makipa bora zaidi na wenye historia nyingi za kuvutia sana na zenye funzo maishani akitokea kwenye familia ya umasikini hadi kuibuka kipa wa dunia kwa sasa.

Kipa huyo alizaliwa Septemba 21, 1992, katika kijiji kidogo cha Sarab-e Yas, kilichopo mkoa wa Lorestan, magharibi mwa Iran ambako ni sehemu ya maeneo maarufu zaidi kwa milima na vijiji vilivyojaa wafugaji.

Akiwa kijana, aliamua kukimbia nyumbani kutoka mkoa wa Lorestan kwenda mji mkuu Tehran ili kutafuta nafasi ya kucheza soka, licha ya kwamba hakuwa na pesa wala mtu mwingine wa kumsaidia ili atimize malengo yake.

Alipofika Tehran, alilala nje ya klabu za soka ambapo alikuwa anaenda kufanya majaribio, huku mara nyingi akilala barabarani kwa sababu alikuwa hana chumba na maisha yake ni ya kulala mtaani na kuhama kila kukicha.

Siku moja alipolala nje ya klabu watu waliopita walifikiri ni ombaomba na walichokifanya ni kumwachia hela pembeni yake na alipoamka alisema ni muda wa kula chakula kizuri ambacho alikuwa hajanunua kutokana na kadhia ya maisha duni aliyopitia maishani.

Baadaye maisha yake yalibadilika kidogo, ambapo alipewa kazi ya muda katika kiwanda cha nguo, kisha kazi katika kioski cha pizza na kuosha magari, japo wakati mwingine alikuwa akienda kulala sehemu zisizokuwa rasmi kabla ya kupata msaada wa watu wa klabu alizokuwa anaenda.

Nyota huyo alianza safari yake ya soka akiwa mshambuliaji kijijini kwao Sarab-e Yas, katika timu za vijana, ila kwenye mechi moja kipa wa timu aliyokuwa anacheza aliumia na hapo ndipo akaamua kuchukua nafasi yake.

Kocha aliyekuwa anafundisha timu za vijana aliamini mchezaji huyo ana uwezo wa kucheza kipa kutokana na kimo chake na uwezo wake, ambapo kuanzia hapo safari yake ya kucheza kipa ikadumu hadi leo hii anapoendelea kuimbwa duniani kote.

Moja ya tukio lililompa heshima ya kujulikana zaidi Beiranvand ni baada ya kuokoa penalti ya mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo katika Fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018, mechi iliyopigwa, Juni 25, 2018 na tangu hapo alijitambulisha ni miongoni mwa makipa bora duniani.

Mwaka 2011, Beiranvand alijiunga na Naft Tehran ambapo alianza kuonekana kimataifa na baadae kusajiliwa na moja ya timu kubwa ya Iran iitwayo Persepolis FC iliyopo Tehran, ambapo alizidi kuonyesha kiwango bora kilichotangaza jina lake.

Kwa sasa, Beiranvand ni kipa namba moja wa timu ya taifa ya Iran, akishiriki Fainali za Kombe la Dunia 2026, ikiwa ni mara ya tatu baada ya awali kushiriki pia mwaka 2018 nchini Urusi na mwaka 2022 pale Qatar.

Beiranvand alishinda tuzo ya kipa bora wa mwaka wa Iran (Persian Gulf Pro League Best Goalkeeper of the Year), mara nne kuanzia msimu wa 2014-2015, 2016-2017, 2017-2018 na

2018-2019, akizidi kuonyesha ni moja ya makipa bora wanaofanya vizuri kwa sasa.

Pia, anashikilia rekodi ya Guinness ya kurusha mpira kwa umbali mrefu wa takribani mita 61.0026 (≈ 61.26 m), aliyoiweka katika mechi ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2018 kati ya Iran dhidi ya Korea Kusini, iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azadi, Tehran, Oktoba 11, 2016.