Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ubelgiji yashikiliwa tena, kipa Iran awabania

Muktasari:

  • Ubora wa makipa umeendelea kudhihirika katika mashindano hayo mwaka huu ambapo kwenye mchezo huo, kipa Alireza Beiranvand wa Iran amefanya kazi bora ya kuzuia mabao ya Ubelgiji.

Ubelgiji bado itaendelea kusubiri kuonja ushindi wake wa kwanza kwenye Fainali za Kombe la Dunia 2026, baada ya kulazimishwa sare ya pili mfululizo, safari hii ikitoka sare tasa na Iran.

Ubora wa makipa umeendelea kudhihirika katika mashindano hayo mwaka huu ambapo kwenye mchezo huo, kipa Alireza Beiranvand wa Iran amefanya kazi bora ya kuzuia mabao ya Ubelgiji.

Ubelgiji imetawala vipindi vyote viwili vya mchezo huo, ikitengeneza mashambulizi mengi lakini Beiranvand mwenye miaka 34 amekuwa mgumu kuruhusu bao kwa kuokoa mashambulizi saba ya wazi.

Ubelgiji itakumbuka nafasi bora zaidi mbili ambazo ya kwanza ni katika  dakika ya 58 wakati pasi ya Kelvin De Bruyne ilipomgonga beki wa Iran kisha mpira kumkuta beki Maxim De Cuyper ambaye alipiga shuti  lililopanguliwa na Beiranvand.

Katika dakika ya 88, Beiranvand akafanya kazi nyingine bora, akipangua shuti la yuleyule De Cuyper na kuifanya Iran iendelee kuikomalia Ubelgiji.

Iran nayo haikuwa nyuma ambapo ilijaribu kutengeneza nafasi kadhaa lakini kama kawaida kizuizi chao kikawa kipa wa Ubelgiji, Thibaut Courtois mwenye miaka 33, aliyefanya kazi nzuri ya kuzuia mashambulizi matatu.

Ubelgiji wakati inatafuta bao la ushindi, imepata pigo baada ya beki wake Nathan Ngoy kupata kadi nyekundu ya moja kwa moja katika dakika ya 66 kwa kosa la kumvuta  mchezaji wa Iran na kuzuia nafasi ya wazi ya kufunga.

Matokeo hayo yanaifanya Iran kuongoza kundi G ikiwa na pointi mbili sawa na Ubelgiji iliyopo nafasi ya pili wakati mchezo mwingine ukisubiriwa kati ya New Zealand dhidi ya Misri.