Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jude Bellingham afunguka kuhusu jeraha

JUDE Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo wa kimataifa wa England aliumia katika dakika ya nane ya mechi dhidi ya Rayo Vallecano Jumapili na haraka akatolewa nje ya uwanja.

MADRID, HISPANIA: STAA wa Real Madrid, Jude Bellingham ametoa ujumbe wa maneno matatu kuhusu maendeleo ya  jeraha lake la msuli wa nyuma ya paja (hamstring) alilopata katika mechi dhidi ya Rayo Vallecano.

Nyota huyo wa kimataifa wa England aliumia katika dakika ya nane ya mechi dhidi ya Rayo Vallecano Jumapili na haraka akatolewa nje ya uwanja.

Bellingham alionekana akitembea kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo huku akilia baada ya kupatiwa matibabu kwenye msuli wa paja la kushoto.

Kiungo huyo sasa anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki nne, jambo litakalomfanya akose mchezo muhimu wa mchujo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Ral Madrid na Benfica.

Kwa upande wa timu ya taifa ya England, Bellingham anatarajiwa kuwa tayari kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki dhidi ya Uruguay na Japan mwishoni mwa Machi.

 Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 sasa ametumia mitandao ya kijamii kuwapa mashabiki taarifa.

Bellingham alichapisha picha ya selfie akiwa amevaa kifaa cha oksijeni na akaandika: “Maisha yanaendelea.”

Baada ya Madrid kushinda 2-1 kutokana na penalti ya dakika za mwisho ya Kylian Mbappe, kocha Alvaro Arbeloa alikiri kwamba “hakuwa na taarifa” yoyote kuhusu jeraha la Bellingham wakati huo kabla klabu ilichapisha ripoti ya madaktari kwenye tovuti yao Jumatatu.

Ripoti hiyo ilisema: “Baada ya vipimo vilivyofanywa leo kwa mchezaji wetu Jude Bellingham na Idara ya Matibabu, imethibitishwa kuwa ana jeraha kwenye msuli wa semitendinosus wa mguu wake wa kushoto.”

Ripoti kutoka Hispania zinaonyesha kuwa atahitaji takribani wiki nne kupona.

Bellingham amecheza mechi 2 tu katika timu ya taifa ya England tangu Agosti mwaka jana. Katika mechi za Septemba, staa huyo aliyelelewa na akademi ya Birmingham City alikuwa bado anauguza upasuaji wa bega.