Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea kuvunja benki kwa Jude Bellingham

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Bellingham amekuwa mhimili muhimu katika kikosi cha Real Madrid tangu ajiunge na klabu hiyo, jambo linalofanya dili hilo kuwa gumu kutimia.

CHELSEA inaripotiwa kupanga kutumia kiasi kikubwa cha hadi Euro 150 milioni kwa lengo la kumsajili kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya England, Jude Bellingham, mwenye umri wa miaka 22.

Bellingham amekuwa mhimili muhimu katika kikosi cha Real Madrid tangu ajiunge na klabu hiyo, jambo linalofanya dili hilo kuwa gumu kutimia.

Hata hivyo, Chelsea inaonekana kuwa tayari kuvunja benki ili kumpata kiungo huyo ambaye anaonekana kufaa katika mradi wao wa kujenga kikosi kipya chenye idadi kubwa ya wachezaji wenye umri mdogo.

Mkataba wa sasa Bellingham unatarajiwa kumalizika mwaka 2029 na tangu kuanza kwa msimu huu, amecheza mechi 27 za michuano yote, amefunga mabao sita na kutoa asisti nne.

Chelsea ina lengo la kimkakati la kujenga safu ya kiungo yeenye nguvu zaidi duniani kwa msimu ujao na kuhakikisha inashinda mataji zaidi.

Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na fundi huyu, hana mpango wa kuondoka kwa sasa ingawa inaaminika Madrid inaweza kuwa tayari kumuuza ikiwa ofa nzuri itawasilishwa mezani kwao.


Cole Palmer

MANCHESTER United imeweka wazi haitomsajili kiungo wa Chelsea na timu ya taifa ya England, Cole Palmer, 23, dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiangazi.

Mabosi wa Man United wanajua thamani ya nyota huyo sokoni iko juu sana na ipo nje ya uwezo wao wa kifedha kwa sasa. Palmer amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu zaidi wa Chelsea, hali inayoongeza thamani yake na kufanya uwezekano wa kuondoka Stamford Bridge kuwa mdogo.


Oleksandr Zinchenko

AJAX ipo mbioni kukamilisha usajili wa moja kwa moja wa kiungo wa Arsenal, Oleksandr Zinchenko, 29.

Zinchenko kwa sasa yuko kwa mkopo Nottingham Forest akitokea Arsenal, lakini Ajax inapambana kumsajili na ipo tayari kutoa Euro 1.5 milioni, pamoja na nyongeza zitakazotegemea na kufuzu kwao Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Nyota huyo mwenye uzoefu mkubwa wa soka la Ulaya anaonekana ni chaguo sahihi kwa Ajax ili kuimarisha safu yao ya kiungo.


Jeremy Jacquet

CHELSEA bado inaendelea na mazungumzo na Rennes kwa lengo la kumsajili beki wa kati wa timu hiyo, Jeremy Jacquet, 20, kabla ya kufungwa dirisha la usajili la Januari.

Matajiri hao wa Jiji la London, wanataka kuimarisha safu yao ya ulinzi na umri wa Jacquet umewavutia sana wakiamini anaendana na mfumo wao.

Mazungumzo bado hayajafikia hatua ya mwisho, lakini Chelsea inaamini kuna uwezekano wa kukamilisha dili.


Diogo Dalot

REAL Madrid inaripotiwa kuwa na nia ya kumsajili beki wa pembeni wa Manchester United, Diogo Dalot, 26.

Vigogo hao wa Hispania wanataka kuziba mapengo yaliyojitokeza katika safu yao ya ulinzi msimu huu na Dalot anaonekana kuwa chaguo sahihi kutokana na uwezo wake wa kucheza pande zote mbili.

Kwa sasa bado haijulikana ikia Man United itakuwa tayari kumruhusu kuondoka kirahisi, hasa ikizingatiwa umuhimu wake.


Davide Frattesi

MABOSI wa Nottingham Forest wamefikia hatua nzuri katika mipango yao ya kumsajili kiungo wa Inter Milan, Davide Frattesi, 26, na ikifeli kumpata dirisha hili itajaribu tena mwisho wa msimu.

Frattesi amekuwa mmoja wa  viungo wanaofanya vizuri Serie A lakini hivi karibuni amekuwa hapati nafasi ya kutosha kikosi cha kwanza hali inayosababisha aangalie uwezekano wa kuondoka na inadaiwa Ligi Kuu England ni sehemu anayohitaji kucheza.


Youssef En-Nesyri

EVERTON imetuma ofa rasmi kwenda Fenerbahce, kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo na Morocco, Youssef En-Nesyri, 28.

Mazungumzo kwa sasa yanaendelea na inaelezwa Everton inataka kumchukua kwa mkopo wenye kipengele cha kumnunua kwa Pauni 17 milioni mwisho wa msimu. En-Nesyri anaonekana kuwa sulihisho la tatizo la mabao Everton.


Patrick Wimmer

EVERTON inaripotiwa inaongoza mbio mbele ya Fulham katika harakati za kumsajili winga wa Wolfsburg, Patrick Wimmer, 24.

Wolfsburg ipo tayari kusikiliza ofa kutoka kwa timu yoyote inayohitaji huduma ya fundi huyo lakini itamuuza kwa dau nono pekee.

Ushindani huu kati ya Everton na Fulham unatarajiwa kuifanya bei ya Wimmer kupanda zaidi na anaweza akauzwa kabla ya dirisha la usajili kufungwa.