Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jude Bellingham azua presha England

JUDE Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo alisikika akipiga kelele kwa maumivu makali baada ya kuanguka chini akiwa na jeraha linaloonekana kuwa baya.

MADRID, HISPANIA: JUDE Bellingham ameshindwa kujizuia na kuangua kulia baada ya kulazimika kutolewa nje kutokana na jeraha la misuli ya paja akiwa na Real Madrid.

Mchezaji huyo wa England, 22, alitolewa kipindi cha kwanza katika mechi ya LaLiga dhidi ya Vallecano.

Na kocha wa timu ya taifa ya England, Thomas Tuchel, atakuwa na hofu kubwa kuwa Bellingham anaweza kukaa nje muda mrefu.

Kiungo huyo alisikika akipiga kelele kwa maumivu makali baada ya kuanguka chini akiwa na jeraha linaloonekana kuwa baya.

Bellingham pia alionekana akishika nyuma ya paja lake kabla ya kuanguka chini na kufuta machozi.

Alibadilishwa na kuingizwa Brahim Diaz baada ya kuwa wazi mara moja kwamba hangeweza kuendelea na mchezo.

Na kocha wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa, hakupunguza hofu juu ya hatima ya Bellingham kuelekea Kombe la Dunia alipozungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari baada ya mechi.

Kocha Arbeloa amesema: “Bado hatujui chochote kuhusu hali ya Bellingham.” Tatizo la misuli ya paja linakuja kama pigo kubwa kwa Tuchel, ambaye anajiandaa kuchagua kikosi chake cha Kombe la Dunia 2026 ndani ya miezi michache ijayo. England inatarajiwa kucheza na Croatia, Ghana na Panama katika hatua ya makundi, huku mechi yao ya kwanza ikipangwa kufanyika Juni 17, 2026.

Tuchel atakuwa akifuatilia kwa karibu ukubwa wa jeraha la Bellingham. Mchezaji huyo wa zamani wa Borussia Dortmund amecheza mechi 28 huko Real Madrid msimu huu, akifunga mabao sita na kuasisti mara nne.

Hata hivyo, umekuwa msimu wenye misukosuko na mashabiki wa vigogo wa LaLiga walimzomea kwa mshangao baada ya kulaumiwa moja kwa moja katika kufukuzwa kwa kocha Xabi Alonso. Licha ya hayo, Real Madrid iliendelea na kuchukua pointi zote tatu dhidi ya Rayo Vallecano, shukrani kwa mabao ya Vinícius Junior na Kylian Mbappe kwenye ushindi wa 2-1.