Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Joto la El Clasico, vipimo kuamua hatma ya Jules Kounde

EL CLASICO Pict

Muktasari:

  • Barcelona imeshakamilisha mazoezi ya mwisho kuelekea mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi wa soka duniani, huku ikianza safari ya kuelekea mjini Madrid kuikabili Real Madrid iliyopania kulipa kisasi cha kupoteza michezo yote ya El Clasico msimu uliopita.

Mabingwa wa Hispania, FC Barcelona, huenda wakamkosa beki wa pembeni kutoka Ufaransa, Jules Kounde, kwenye mechi ya El Clasico, itakayopigwa kesho Jumapili, Oktoba 26, 2025 kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid.

Barcelona imeshakamilisha mazoezi ya mwisho kuelekea mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi wa soka duniani, huku ikianza safari ya kuelekea mjini Madrid kuikabili Real Madrid iliyopania kulipa kisasi cha kupoteza michezo yote ya El Clasico msimu uliopita.

Kounde ameibua sintofamu ya kuwa kwenye kiksoi cha Barcelona kitakachopambana ugenini, kufuatia kukosa mazoezi ya pamoja kwa siku ya Alhamisi na Ijumaa kutokana na majeraha madogo aliyopata.

EL 01

Kounde alipata majeraha madogo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya siku ya Jumanne Oktoba 21, 2025, Barcelona ilipocheza dhidi ya Olympiacos ya Ugiriki.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka SPORT, Kounde aliwasili kwenye kituo cha mazoezi cha Ciutat Esportiva mapema leo Jumamosi Oktoba 25, 2025 saa 3:15 asubuhi, muda uleule ambao wachezaji wengine waliitwa kwa ajili ya mazoezi ya mwisho yaliyoanza saa 4:30 asubuhi.

Kocha Hansi Flick aliweka muda wa mwisho wa kufika saa 3:30 asubuhi, na ujio wa Kounde mapema ulionyesha maendeleo mazuri katika hali yake, tofauti na siku zilizopita ambapo hakuwa anafanya mazoezi na wenzake.

EL 02

Hata hivyo, vipimo vya mwisho kabla ya mechi dhidi ya Real Madrid, vitatoa majibu kamili kama Kounde ataweza kucheza kesho, licha ya kuwa taarifa zingine zinaeleza kocha Flick anahofia kumtumia kwa kuhatarisha hali yake.

Wakati huo huo, Frenkie de Jong na Andreas Christensen wote wamepona kikamilifu majeraha yaliyokuwa yanawasumbua, na wana uhakika wa kuwa sehemu ya kikosi cha Barcelona kesho Jumapili.

Wakati wawili hao wakitarajiwa kucheza mechi hiyo, kiungo kutoka Brazil Raphinha hatokuwepo kabisa.