Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Joshua, Wilder ngoma inapigwa

JOCHUA Pict

Muktasari:

  • Wilder na Joshua hawajawahi kupigana na hivyo hakuna matokeo ya pambano kati yao.

LONDON, ENGLAND: BONDIA Deontay Wilder anaweza kupigana na Anthony Joshua ‘AJ’ ikidaiwa kwamba majadiliano yamefikia hatua nzuri ili wawili hao wazichape hivi karibuni.

Wilder na Joshua hawajawahi kupigana na hivyo hakuna matokeo ya pambano kati yao.

Hata hivyo, wote waliwahi kuwa mabingwa wa uzito wa juu na waliwahi kushinda mapambano makubwa sambamba na vipigo tofauti katika maisha yao ya ngumi.

Meneja wa Joshua, Eddie Hearn anasema kwamba Wilder ana uwezekano mkubwa kuzichapa na bondia wake na kwamba, mpango mzima utajulikana atapokutana na Tyrrell Herndon huko Kansas, Marekani mwezi ujao.

Wilder alipoteza mechi nne kati ya tano za mwisho na alipigwa kwa mshangao na bondia wa China, Zhilei Zhang, Juni mwaka jana. Hii ilikuja miezi sita baada ya kumalizana na Joseph Parker tukio lililozuia lile dhidi ya ‘AJ’.

Akizungumza na FightHype.com, Hearn amethibitisha kuwa Wilder amesaini kupigana na Joshua na tangazo linatarajiwa kutolewa karibuni.

Hearn anaamini kuwa Wilder amepoteza hofu aliyokuwa nayo katika ulingo, lakini alibainisha kuwa mechi na Joshua  inaweza kutokea baadaye.

“Kama (Wilder) ataendelea kushinda, labda watu wanaweza kuzungumzia mechi hiyo, lakini niwahakikishie kwamba anazichapa hivi karibuni na Joshua,” alisema Hearn.

“Hii si mechi ambayo naikataa, lakini watu hawampi Wilder nafasi kubwa dhidi ya AJ kwa sasa, lakini tunalo tumaini ataanza kuonekana vizuri tena.

“Tunazungumzia mabondia kupoteza mwelekeo. Huu ni mfano mzuri. Ni wa kuchekesha jinsi watu walivyokuwa na hofu  ya mchezaji mmoja, na kisha ghafla hawana hofu.

“Sasa, siamini mtu yeyote atahofu kupigana na Deontay Wilder wakati zamani kila mtu aliogopa. Sasa, kila mtu anataka kupigana naye.”

Hearn pia alitaja kuwa kipigo cha mwisho cha Joshua ulingoni kinafanya mechi na Wilder iwezekane zaidi kwani wote wana usongo wa kutafuta mafanikio mapya.

Ndoto za AJ kuwa bingwa wa uzito wa juu zilipotea baada ya kushangazwa na kichapo cha Daniel Dubois katika Uwanja wa Wembley, Septemba, mwaka jana.

Dubois sasa anakutana na Oleksandr Usyk katika uwanja huo huo Julai, mwaka huu akiwania kuwa bingwa wa uzito wa juu wa Uingereza tangu Lennox Lewis alipofanya hivyo.

Wilder, kwa upande wake, anakosolewa tangu aliposhindwa na Zhang, ambapo mashabiki wengi wa ngumi wanamtaka ajeree ulingoni.

“Mechi hii haitakuwa na mambo mengi, isipokuwa (Wilder) kupata tena imani kupitia ushindi,” alisema Hearn.

“Kama atashindwa na huyu jamaa basi aache, lakini natarajia ashinde na kwa matumaini ashinde vizuri.”