Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jamie Carragher ataja kumi wenye uhakika England

CARRA Pict

Muktasari:

  • Three Lions inajiandaa kwa mashindano makubwa yatakayofanyika Marekani, Mexico na Canada majira ya kiangazi baada ya kujua wapinzani wao katika hatua ya makundi. Kocha, Thomas Tuchel anatarajia kumaliza miaka 60 ya maumivu kwa kusaidia England kushinda kombe lao la kwanza la Dunia tangu mwaka 1966.

LONDON, ENGLAND: JAMIE Carragher amewaacha Cole Palmer na Phil Foden kwenye orodha yake ya wachezaji kumi wa "uhakika" wa timu ya taifa ya England kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2026.

Three Lions inajiandaa kwa mashindano makubwa yatakayofanyika Marekani, Mexico na Canada majira ya kiangazi baada ya kujua wapinzani wao katika hatua ya makundi. Kocha, Thomas Tuchel anatarajia kumaliza miaka 60 ya maumivu kwa kusaidia England kushinda kombe lao la kwanza la Dunia tangu mwaka 1966.

Kocha huyo Mjerumani anakabiliwa na maamuzi magumu, hasa kutokana na wingi wa vipaji vinavyocheza nafasi zinazofanana.

CAR 01

Na gwiji wa Liverpool, Carragher, anaamini ni wachezaji 10 tu wanaopaswa kuwa na uhakika wa moja kwa moja wa nafasi. Chaguo lake ni Jordan Pickford, Reece James, Ezri Konsa, Marc Guehi, Elliot Anderson, Declan Rice, Morgan Rogers, Jude Bellingham, Bukayo Saka na Harry Kane.

Hata hivyo, jina kubwa zaidi aliloacha ni nyota wa Chelsea, Cole Palmer, ambaye amekuwa na msimu wenye changamoto kutokana na majeraha.

Pia hakumtaja Phil Foden wa Manchester City na winga wa Barcelona, Marcus Rashford.

CAR 02

Baadaye, Carragher alifichua kikosi chake kamili cha wachezaji 26 kwa Kombe la Dunia 2026 na Palmer, Foden pamoja na Rashford wote walijumuishwa, licha kwamba hawapo kwenye ile orodha ya wachezaji wake 10 wenye uhakika zaidi wa kupata nafasi.

Hakukuwa na mshangao mkubwa, lakini John Stones aliachwa kwenye safu ya ulinzi, pamoja na Nico O’Reilly wa Man City.

Katikati ya uwanja, alimjumuisha kiungo mkongwe wa zamani wa Liverpool, Jordan Henderson pamoja na Kobbie Mainoo aliyerudi katika kiwango bora.

Lakini kwa kuwa Palmer, Bellingham, Foden na Morgan Rogers wote walikuwa kwenye kikosi chake, alilazimika kumwacha Eberechi Eze wa Arsenal.

CAR 03

Katika safu ya ushambuliaji, Harry Kane na Ollie Watkins walikuwa washambuliaji wake pekee, jambo lililomwacha nje Dominic Calvert-Lewin.

Akielezea chaguzi zake, Carragher alizungumzia Palmer, Foden na changamoto anayokumbana nayo Tuchel katika safu ya mbele.

Amesema: “Cole Palmer si wa uhakika, lakini ni mchezaji wa ajabu sana. Mambo hayajaenda vizuri Chelsea kutokana na majeraha, lakini kumbukeni kiwango chake dhidi ya PSG kwenye fainali ya Kombe la Dunia la Klabu. Alikuwa wa kipekee kabisa. Amefunga bao kwenye fainali (kwa England, Euro 2024).

“Kwa upande wangu, Phil Foden pia anaenda. Lakini huwezi kuwachezesha wote wawili (Foden na Palmer) kwenye timu moja. Kuhusu Rashford, nilikuwa na uamuzi mgumu, sidhani kama wale waliokuwa nje wamefanya vya kutosha.

“Niliamua kumchukua Anthony Gordon amekuwa chaguo la kuaminika. Anahitaji kuongeza mabao, lakini nimemchagua mbele ya (Noni) Madueke, ambaye sidhani kama atapata muda wa kucheza wa kutosha.”