Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carragher ataja makocha wanne wanaofaa Man United

Muktasari:

  • Carrick ana miezi minne ya kuwavutia mabosi wa Old Trafford baada ya kupewa jukumu la ukocha wa muda hadi mwisho wa msimu huu.

MANCHESTER, ENGLAND: GWIJI wa Liverpool na mchambuzi wa soka, Jamie Carragher amesema haamini kama Michael Carrick ana ubora huo unaohitajika kupata kazi ya ukocha wa kudumu katika klabu ya Manchester United, lakini akitaja makocha wanne anaowaona wanafaa kuchukua kibarua hicho na mambo yatakuwa matamu.

Carrick ana miezi minne ya kuwavutia mabosi wa Old Trafford baada ya kupewa jukumu la ukocha wa muda hadi mwisho wa msimu huu.

Na aliweza kuanza kibarua chake vizuri zaidi kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mahasimu wao wa jadi Manchester City kwenye dabi ya Manchester Jumamosi uliyopita, ikiwa ni ushindi uliopatikana kwa ufundi wake mwenyewe.

Hata hivyo, Carragher bado anaamini kuwa Mashetani Wekundu wanapaswa kumwangalia mmoja kati ya Thomas Tuchel, Julian Nagelsmann, Eddie Howe au Luis Enrique kama kocha wa kudumu katika kikosi hicho cha Old Trafford kwa ajili ya msimu ujao.

Akizungumza kwenye Monday Night Football, Carra alisema: “Siamini Manchester United wanaweza kushinda ligi wakiwa na Michael Carrick kama kocha. Sijaribu kumkosea heshima. Lazima uwe wa kipekee sana. Fikiria makocha waliowahi kushinda Ligi Kuu England, asilimia 99 yao ni wa kipekee, na nadhani Michael Carrick anakosa sifa hiyo. Huenda nikathibitishwa kuwa nimekosea, lakini hiyo ndiyo sababu namwondoa Michael Carrick kwenye orodha ya wagombea.”

Man United ilimfuta kazi kocha wao wa sita wa kudumu tangu Sir Alex Ferguson astaafu, walipoamua kumtimua Ruben Amorim mapema mwezi huu.

Kocha huyo wa Ureno aliwasili Old Trafford akiwa na sifa kubwa, lakini utawala wake ulivunjika baada ya muda mfupi wa zaidi ya mwaka mmoja.

Carragher aliwaondoa majina makubwa kadhaa alipopewa orodha ya makocha 25 wanaoweza kumrithi Amorim kwenye benchi la ufundi la Man United.

Carlo Ancelotti, Mauricio Pochettino, Gareth Southgate, Xabi Alonso, Enzo Maresca, Zinedine Zidane na Oliver Glasner wote walionekana kutofaa kwa mujibu wa gwiji huyo wa Liverpool na beki wa zamani wa Ligi Kuu England.

Katika mchezo wa dabi, Bryan Mbeumo alivunja ukame wa mabao dakika ya 65 baada ya Man United kugomewa mabao mawili kipindi cha kwanza kwa madai ya matukio ya kuotea. Patrick Dorgu kisha aliwafanya mashabiki wa Old Trafford walipuke kwa shangwe la furaha baada ya kutumia kosa la Rico Lewis dakika ya 76 kwa kuiwahi krosi ya Matheus Cunha na kuutumbukiza moira nyavuni.

Mchezaji aliyetokea benchini Mason Mount alidhani amekamilisha ushindi huo mkubwa, lakini uchambuzi mrefu wa VAR ulifuta bao la tatu.

Kocha wa zamani wa Chelsea, Thomas Tuchel, ambaye ataiongoza timu ya taifa ya England kwenye Kombe la Dunia 2026, ndiye chaguo kuu la Carragher.

Anaamini Mjerumani huyo ana nguvu na hamasa za kufanikiwa, angepigania timu yake hadi mwisho, na ana nafasi nzuri ya kupata kazi hiyo.

Carragher pia anaamini kuwa kocha wa Ujerumani, Julian Nagelsmann anaweza kuwa chaguo zuri kwa kuwa ana kitu cha kuthibitisha baada ya kazi yake ya mwisho ya klabu huko Bayern Munich kuisha vibaya ndani ya miaka miwili.

Kocha wa Newcastle, Eddie Howe, yuko juu kwenye orodha ya Carragher kutokana na mtindo wake wa uchezaji na uwezo wake wa kukabiliana na vyombo vya habari. Na kocha wa Paris Saint-Germain, Luis Enrique, anakamilisha orodha ya makocha wanne, akiwa ni kocha ambaye Carragher anaamini kila mtu atamtaka wakati wa majira yajayo ya kiangazi baada ya kuonekana kuwa tayari kwenda kukabiliana na changamoto mpya.