Jake kumrudisha ulingoni Anthony Joshua, kuzichapa Desemba 2025
Muktasari:
- Kwa mujibu wa The Daily Mail, kambi za mabondia hao zinaripotiwa kuwa karibu kufikia makubaliano katika mazungumzo kabla ya uamuzi wa mwisho wa kumaliza ubishi ulingoni Desemba 9 au 12.
Bondia wa England, Anthony Joshua anatarajia kupambana na Jake Paul kutoka Marekani katika pambano kubwa la uzani wa juu litakalofanyika mjini Miami mapema mwezi Desemba 2025.
Kwa mujibu wa The Daily Mail, kambi za mabondia hao zinaripotiwa kuwa karibu kufikia makubaliano katika mazungumzo kabla ya uamuzi wa mwisho wa kumaliza ubishi ulingoni Desemba 9 au 12.
Awali, Paul alitarajiwa kupigana na mpinzani wake kutoka Marekani, Davis, Jumamosi Novemba 16, 2025, lakini pambano hilo lilifutwa kufuatia tuhuma za unyanyasaji wa majumbani zinazomkabili Davis.
Joshua hajawahi kupanda ulingoni tangu alipochapwa na mpinzani wake wa England, Daniel Dubois, mwaka 2024.
Dubois alimchapa Joshua kwa knockout katika raundi ya tano, jambo lililozima matumaini ya bondia huyo mwenye umri wa miaka 36, ya kurejea katika mbio za kuwania mataji ya uzani wa juu duniani.
Anthony Joshua ni bondia wa uzani wa juu ambaye amejizolea umaarufu mkubwa duniani kutokana na mafanikio yake ulingoni.
Alianza kucheza ngumi za kulipwa mwaka 2013 baada ya kushinda medali ya dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki ya London mwaka 2012. Joshua alipata umaarufu zaidi mwaka 2017 alipoibuka mshindi dhidi ya bingwa wa muda mrefu, Wladimir Klitschko, pambano lililompa mataji ya dunia ya IBF, WBA, na IBO.
Amewahi kuwania na kushikilia mataji hayo mara kadhaa, akipambana na mabondia wenye majina makubwa kama Andy Ruiz Jr, ambaye alimshinda mwaka 2019 na kurejesha mataji aliyoyapoteza. Ingawa amepitia vikwazo, ikiwemo kupoteza kwa Daniel Dubois mwaka 2024, Joshua bado anabaki kuwa mmoja wa mabondia wanaoheshimika zaidi katika historia ya ndondi za kisasa.
Kwa upande wa Jake Paul, ni bondia ambaye alianza kama nyota wa mitandao ya kijamii kabla ya kuingia rasmi kwenye ndondi mwaka 2020. Akiwa na historia ya umaarufu kupitia YouTube na televisheni.
Jake alitumia jina lake kujenga taaluma ya ndondi za kulipwa, akivutia watazamaji wengi duniani. Amejipatia umaarufu kwa kupigana na wanamichezo na watu mashuhuri kutoka fani mbalimbali, wakiwemo wanandondi wastaafu kupitia michuano ya UFC kama Tyron Woodley na Anderson Silva, wote aliowashinda.
Licha ya kukosolewa na baadhi ya mashabiki kwa kuanza ndondi kupitia njia isiyo ya siyo ya kawaida, Jake Paul ameonyesha uwezo na kujituma, akijenga hadhi kama mmoja wa mabondia wapya wanaovutia zaidi katika kizazi kipya cha ndondi. kawaida, bondia huyu ameonyesha uwezo na kujituma, akijenga hadhi kama mmoja wa mabondia wapya wanaovutia zaidi katika kizazi kipya cha ndondi.