Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Isak ni balaa jingine

ISAK Pict

Muktasari:

  • Kocha hiyo anaamini kwamba wamepata mmoja wa washambuliaji bora zaidi duniani ambaye wamemsajili akitokea Newcastle kwa ada iliyoweka rekodi ya usajili ya Pauni 125 milioni.

LIVERPOOL, ENGLAND: MMESIKIA!? Arne Slot kocha Liverpool, anaamini staa wao, Alexander Isak, ataweza kuwa mshambuliaji bora zaidi duniani iwapo tu atashinda makombe makubwa.

Kocha hiyo anaamini kwamba wamepata mmoja wa washambuliaji bora zaidi duniani ambaye wamemsajili akitokea Newcastle kwa ada iliyoweka rekodi ya usajili ya Pauni 125 milioni.

Hata hivyo, anasisitiza kwamba namba tisa huyo mpya wa Liverpool lazima anyakue makombe makubwa kama Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kutajwa kuwa bora.

Alipoulizwa kama Isak ndiye mshambuliaji bora zaidi duniani, Slot alisema: "Ndio ni mmoja wao. Ila kwa sasa siyo, sababu ni kwamba amekuwa nje kwa miezi minne. Ikiwa utaandika nimesema si bora duniani, lazima uongeze kipengele hicho, la sivyo haitakuwa sahihi kabisa, kwa sababu yeye ni mmoja wa washambuliaji bora. Lakini ili awe bora kuliko wote, nafikiri wachezaji bora zaidi duniani hushinda makombe, na hiyo ndiyo tunachohitaji sisi na yeye kufanya."

Mshambuliaji huyo wa Sweden tayari ameonyesha uwezo wake kwa kufunga mabao 54 ya Ligi Kuu ndani ya misimu mitatu akiwa na Newcastle, na pia kuisaidia klabu hiyo kufika fainali ya Carabao Cup msimu uliopita, ambapo ilishinda dhidi ya Liverpool.

Lakini sasa anakabiliwa na shinikizo jipya la kuchezea Liverpool na kuonyesha thamani sawa ya bei kubwa ya usajili wa rekodi ya Uingereza ambayo timu hiyo ilivunja kwa ajili ya kumpata.

"Watu wanaweza kumwekea shinikizo na presha ili afanye vizuri, lakini hilo haliwezi kuwa jambo jipya, kwa sababu ukiwa na nembo hii kifuani (anaonyesha nembo ya Liverpool), shinikizo siku zote lipo. Hata kama tusingemsajili, bado mngekuwa mnanitarajia kushindania ubingwa wa ligi, hivyo shinikizo hili siku zote lipo.

"Kuhusu pesa nyingi zilizotumika kwa mchezaji mmoja, hilo pia ni tabia zetu. Siyo mara ya kwanza kufanya hivi. Hata kabla sijafika hapa, uongozi ulifanya hivyo kwa Virgil van Dijk, kwa Alisson Becker. Huwa tunaangalia mchezaji, tunayetaka kumpata. Tukimhitaji na kuona thamani yake huwa hatusiti kuchukua hatua. Fedha hizo tunazirudisha kwa kufanya biashara ya wachezaji wengine na kushinda ubingwa."