Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Isaak ni mashine ya hela

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya Anfield imefanya mawasiliano rasmi na mabosi wa Newcastle kuwaambia dhamira yao ya kulipa Pauni 120 milioni kwa ajili ya kunasa saini ya straika huyo mashine ya mabao Isak, 25.

LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL ipo tayari kuvunja rekodi ya Uingereza kwenye uhamisho wa wanasoka kwa kumnasa straika wa Newcastle United na Sweden, Alexander Isak.

Miamba hiyo ya Anfield imefanya mawasiliano rasmi na mabosi wa Newcastle kuwaambia dhamira yao ya kulipa Pauni 120 milioni kwa ajili ya kunasa saini ya straika huyo mashine ya mabao Isak, 25.

Liverpool bado haijaweka rasmi ofa yao mezani ikiwasubiri mabosi wa St James’ Park kujibu kwanza kama wapo tayari kwa jili ya kufanya dili hilo.

Newcastle, ambao wameshuhudia ofa yao ya Pauni 69.5 milioni waliyopeleka huko Frankfurt wakimtaka straika Hugo Etitike ikikataliwa na timu hiyo ya Ujerumani, imeweka wazi haina mpango wa kumuuza Isak, ambaye amefunga mabao 54 katika mechi 86 alizocheza kwenye Ligi Kuu England tangu alipotua kwenye timu hiyo akitokea Sociedad kwa ada ya Pauni 63 milioni mwaka 2022.

Lakini, wakati Isak akiwa hana mpango wowote wa kulazimimisha uhamisho, kinachoelezwa ni kwamba atafurahia kwenda kuungana na mabingwa hao wa Ligi Kuu England.

Na kinachoelezwa kingine ni kwamba Liverpool imewatishia Newcastle kwamba itavamia kwenye mawindo yao ya straika Etitike endapo kama watashindwa kumpata mtu wanayemtaka, Isak.

Mchakato huo umekuja wakati Liverpool ikiigomea pia Bayern Munich na ofa yao ya Pauni 58.6 milioni kwa ajili ya kunasa huduma ya winga Mcolombia, Luis Diaz.

Liverpool imegomea ofa hiyo kwa sababu imelenga kupata mkwanja mrefu zaidi kutoka AC Milan au Al Hilal ya Saudi Arabia kutokana na kuhitaji saini ya mshambuliaji wa Uruguay, Darwin Nunez.

Newcastle inaaminika kumthaminisha mshambuliaji Isak kuwa na thamani ya Pauni 150 milioni, kiwango cha pesa ambacho hata Liverpool haitaweza kukifikia. Lakini, inaweza kukubali ofa chini ya hapo, endapo kama itakuwa pesa inayotosha kwa wao kufikia bei anayouzwa Etitike ya Pauni 85 milioni. Lakini, taarifa inayoripotiwa na SunSport ni kwamba Newcastle imeiambia Liverpool mchezaji Isak hauzwi kwa dau lolote lile. Mkataba wa Isak huko Newcastle utafika tamati 2028 na kuna mazungumzo ya kuboreshewa mshahara wake na hilo linaweza kutokea ndani ya wiki chache zijazo.