Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ile siku ya fainali UEFA CL ndo leo

UEFA Pict

Muktasari:

  • Hii itakuwa ni fainali ya pili kwa Inter MIlan ndani ya Jiji la Munich kwani iliwahi kucheza awali mwaka 1965, wakati huo michuano ikiitwa European Cup na kukutana na Benfica.

MUNICH, UJERUMANI: ILE siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu ndio leo. Ndio, leo ni kilele cha michuano ya kimataifa Ulaya kwa msimu huu. Mechi kubwa ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inapigwa  leo katika nchi inayoshika nafasi ya nne kwa kuzalisha asali barani Ulaya,  Ujerumani.

Mechi hii itapigwa kwenye Uwanja wa Allianz Arena, jijini Munich kuanzia Saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki.

Hii itakuwa ni fainali ya pili kwa Inter MIlan ndani ya Jiji la Munich kwani iliwahi kucheza awali mwaka 1965, wakati huo michuano ikiitwa European Cup na kukutana na Benfica.


Hapa chini kuna takwimu na mambo muhimu ya kufahamu kuelekea mchezo huo.

UE 01

Paris SaintGermain (PSG)

Kocha: Luis Enrique

Msimu huu: PSG imetawala Ligi Kuu Ufaransa na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili baada ya ile ya 2020.

Wachezaji muhimu: Gianluigi Donnarumma (kipa), Achraf Hakimi, Nuno Mendes, Vitinha, Fabian Ruiz, Joao Neves, Ousmane Dembele, Khvicha Kvaratskhelia.

Uchezaji: PSG imejikita zaidi katika kucheza soka la aina ya Tik-Tak.

UE 02

Inter Milan

Kocha: Simeone Inzaghi

Wachezaji tegemeo: Yann Sommer (kipa), Alessandro Bastoni, Francesco Acerbi, Hakan Calhanoglu, Nicolo Barella, Lautaro Martinez na Marcus Thuram.

Mbinu za uchezaji: Inter inajivunia mbinu mathubuti za ulinzi na mashambulizi ya haraka ikitumia vyema mipira ya kona na makosa.

UE 03

TAKWIMU MUHIMU

Kipengele                      PSG                      Inter Milan

Mabao yaliyofungwa      15                             11

 Clean Sheets                  8                                7

Asilimia umiliki             51.2                           50.6

Usahihi pasi                   88.3                           87.7

Kadi za njano                  20                             16

Kadi nyekundu               0                                 0

Mipira ya kona                29                               19

Mipira ya penalti             5                                  3

Fainali                            1 (kabla ya 2025)        6 (kabla ya 2025)

Mataji ya UCL                0                                     3


ZAWADI

Shirikisho la Soka Afrika lilitenga Euro 914 milioni kama mgawo wa zawadi kwa timu zote zinazoshiriki katika mashindano hayo kwa kuzingatia mafanikio.

Mshindi ama ni iwe PSG au Inter Milan itapata Euro 25 milioni (takriban Sh73.2 bilioni) ilhali mshindi wa pili atapata Euro 18.5 milioni (takriban Sh 54.2 bilioni).

Mbali na zawadi ya fainali timu zote zimekusanya mapato kupitia hatua mbalimbali za mashindano kwa kuanza na PSG hadi sasa tayari imeshaingiza Euro 76.14 milioni ambazo zimetokana na malipo ya ushiriki, ushindi wa mechi za na makundi na mtoano.

Kwa upande wa Inter Milan kwa mujibu wa tovuti ya Football365 imeshakusanya Euro 74.49 milioni hadi sasa.

Kwa ujumla kwa timu itakayofanikiwa kushinda taji inaweza kujikusanyia Euro 101 milioni ambazo ni zaidi ya Sh296 bilioni.

UE 04

REKODI ZAO

Timu hizo zimekutana mara mbili katika michuano tofauti, lakini hazijawahi kukutana katika michuano hiyo.

Mara ya kwanza ilikuwa ni Desemba, 30, 2015 huko  Doha nchini Qatar ambapo mechi ilimalizika kwa Inter Milan kushinda kwa mabao 2-1.

Mechi hiyo ilikuwa ni ya kirafiki kama sehemu ya maandalizi ya katikati ya msimu wa mashindano.

Makocha walitumia nafasi hiyo kuwajaribu wachezaji chipukizi waliokuwa nao vikosini. Mara ya pili zilikutana Julai, 27, 2019 katika michuano ya  International Champions Cup iliyopigwa huko Shenzhen, China ambapo dakika 90 zilimalizika kwa sare ya bao 1-1 na PSG ikaenda kushinda kwa penalti 6-5.

Mechi hiyo ilichezwa wakati wa maandalizi ya msimu mpya.


WAAMUZI

Mwamuzi: Szymon Marciniak (Poland)

Kibendera 1: Tomasz Listkiewicz (Poland)

Mwamuzi wa akiba: Pawel Sokolnicki (Poland)

Mwamuzi wa VAR: Danny Makkelie (Uholanzi)

Msaidizi wa VAR: Pol van Boekel (Uholanzi)

Msaidizi wa VAR: Kevin Blom (Uholanzi).