Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zidane akataa ofa kubwa Saudi Arabia

ZIDANE Pict
ZIDANE Pict

Muktasari:

  • Mfaransa huyo hajawahi kuwa na jukumu la ukocha tangu alipomaliza kipindi chake cha pili akiwa na Madrid katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka 2021.

PARIS, UFARANSA: KOCHA wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane amekataa nafasi ya kurejea katika ukocha licha ya kutokuwa na kazi kwa miaka minne.

Mfaransa huyo hajawahi kuwa na jukumu la ukocha tangu alipomaliza kipindi chake cha pili akiwa na Madrid katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka 2021.

Tangu hapo amehusishwa na timu  mbalimbali, ikiwamo Manchester United, Chelsea, na timu ya taifa ya Ufaransa, lakini hadi sasa ameamua kusalia nje ya soka.

Gazeti la Marca liliripoti mapema mwaka huu kuwa Zidane angerudi tu katika ukocha endapo angepata nafasi ya kuifundisha tena Real Madrid au timu ya taifa ya Ufaransa.

Nafasi ya Real Madrid tayari imechukuliwa na kiungo wa zamani wa timu hiyo, Xabi Alonso, huku ajira ya Ufaransa itapatikana mwakani wakati Didier Deschamps atakapoachia ngazi baada ya Kombe la Dunia 2026.

Kutokana na hali hiyo, kwa mujibu wa tovuti ya L’Équipe, Zidane amekataa mkataba wa mnono wa mwaka mmoja wenye thamani ya Euro 100 milioni kutoka kwa timu ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia.

Timu iliyotoa ofa hiyo haikutajwa, ingawa kuna timu kadhaa ikiwamo Al Hilal inayoshiriki Kombe la Dunia la Klabu ambazo kwa sasa zinatafuta kocha.

L’Équipe iliongeza kuwa kiungo huyo wa zamani bado anajikita katika kuchukua nafasi ya Deschamps kama kocha wa Ufaransa ambapo anaweza kuweka rekodi ya kushinda Kombe la Dunia akiwa mchezaji na kocha wa timu hiyo katika nyakati tofauti ambapo kwa sasa Deschamps,  Mario Zagallo na Franz Beckenbauer wamewahi kuiweka.

Awali, Zidane alisema kwa sasa hana mpango  wa kufanya kazi katika timu yoyote ya England kwa kuwa hajui lugha ya Kiingereza kwa ufasaha.

“Kuhusu Manchester? shida ninaelewa Kiingereza, lakini siwezi kuzungumza kwa ufasaha.”