Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Henry ataka bao la ugenini lirudi Ulaya

HENRY Pict

Muktasari:

  • Inter Milan ilikaribia kabisa kushinda kupata ushindi wao kihistoria baada ya staa wa zamani wa Arsenal na Manchester United, Henrikh Mkhitaryan kufunga bao ambalo lingekuwa la nne kwenye dakika za mwisho za kipindi cha pili, lakini VAR ililikataa kwa kuwa mfungaji aliotea.

LONDON, ENGLAND: SUPASTAA Thierry Henry amesema angependa kuona sheria ya bao la ugenini irudishwe baada ya Barcelona na Inter Milan kufungana mabao 3-3 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyofanyika Hispania, Jumatano iliyopita.

Inter Milan ilikaribia kabisa kushinda kupata ushindi wao kihistoria baada ya staa wa zamani wa Arsenal na Manchester United, Henrikh Mkhitaryan kufunga bao ambalo lingekuwa la nne kwenye dakika za mwisho za kipindi cha pili, lakini VAR ililikataa kwa kuwa mfungaji aliotea.

VAR ilionyesha Mkhitaryan amezidi vidole vya mguu tu na kufanya mechi hiyo ilimalizike kwa matokeo hayo ya sare ya 3-3 na kusubiriwa marudiano yatakayofanyika San Siro, Jumanne ijayo.

Barcelona ilipambana kusawazisha mara mbili baada ya kutanguliwa kwa mabao mawili ya haraka kutoka kwa Marcus Thuram, aliyefunga kwa kisigino na Denzel Dumfries kwa ticktack.

Lakini, Lamine Yamal alifunga bao matata kabisa, kabla ya Ferran Torres kuisawazishia Barcelona kabla ya mapumziko. Kipindi cha pili, Dumfries alifunga bao lake la pili na tatu kwa Inter, hivyo kuifanya Barcelona kulazimika tena kutokea nyuma na safari hii ni Raphinha, ndiye aliyesawazisha kwa shuti kali.

Baada ya viwango bora kabisa kutoka kwa timu zote, Henry alisema Inter Milan ilipaswa kufaidika kutokana na kiwango chao.

Akizungumzia sheria ya bao la ugenini, Henry alisema: "Najua ilikuwa ikitumika kwa muda mrefu na sote tuliikubali. Lakini, nje ya hapo nilizungumza na Jamie (Carragher), inakuwaje unafunga mabao matatu ugenini na usiwe na faida? Mabao ya ugenini yalikuwa muhimu sana kwangu, lakini sasa unafunga mabao maatu ugenini na bado hakuna faida yoyote ukirudi kucheza nyumbani unaanza 0-0."

Sheria hiyo ilifutwa na Uefa mwaka 2021. Kipindi Kocha Arsene Wenger alipokuwa akiinoa Arsenal alidai bao la ugenini limepewa uzito mkubwa sana kwa sababu lilikuwa likiifanya timu ya nyumbani kucheza kwa tahadhali sana.

Kwa kutokuwapo kwenye sheria hiyo, ina maana nusu fainali hiyo inaweza kuingia kwenye dakika 30 za nyongeza au penalti kama timu hizo zitashindwa kufungana kwenye mechi ya marudiano, hivyo mabao matatu iliyofunga Inter ugenini, hayana faida yoyote kwao.


Kwanini sheria ya bao la ugenini ilifutwa?

Sheria hiyo ilifutwa baada ya mapendekezo kutoka kwenye Kamati ya Mashindano ya Uefa na ile Kamati ya Soka ya Wanawake. Kwamba mechi ya mtoano ya michuano ya Ulaya iliyomalizika kwa timu kulingana kwenye mechi zote mbili, zitalazimika kucheza dakika 30 za ziada na kisha kama hakutakuwa na mshindi, zitapigwa penalti.

Rais wa Uefa, Aleksander Ceferin alihoji uhalali wa sheria hiyo na kuamini ilikuwa ikiifanya timu ya nyumbani iliyopata bao la ugenini kwenye mechi ya kwanza isifanye mashambulizi katika mechi ya marudiano.

Sheria ya bao la ugenini ilikuwa ikitumika kwenye michuano ya Uefa tangu mwaka 1965, lakini sasa imefutwa jambo ambalo kuna baadhi ya wadau akiwamo Henry kutamani irudishwe.

Utafiti wa Uefa kabla ya kuchukua uamuzi huo ni kwamba ushindi wa timu za nyumbani zilizopata bao kwenye mechi za kwanza za ugenini ulishuka kutoka asilimia 61 kwenye miaka ya 1970 hadi asilimia 47 katika msimu wa 2020-21.

Na wastani wa mabao kwa mechi za nyumbani ulishuka kutoka 2.01 hadi 1.58 - kwa sababu timu iliyopata bao la ugenini, iliporudi nyumbani iliweka mkazo zaidi kwenye kujilinda kuliko kushambulia na hivyo kuwanyima uhondo mashabiki.