Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Antony hashikiki huko Real Betis

ANTONY Pict

Muktasari:

  • Mbrazili huyo alifunga bao matata kabisa katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Fiorentina katika nusu fainali ya kwanza ya Europa Conference League, Alhamisi iliyopita.

SEVILLE, HISPANIA: GWIJI wa Hispania, Joaquin amepanga "kumteka" Antony ili kumzuia winga huyo kurudi Manchester United.

Mbrazili huyo alifunga bao matata kabisa katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Fiorentina katika nusu fainali ya kwanza ya Europa Conference League, Alhamisi iliyopita.

Baada ya kupata mpira nje ya 18, Antony alijaribu kupiga shuti kwa guu la kushoto, akashindwa kabla ya kuwahi mpira huo na kuupiga kwa mguu wa kulia, mpira huo ukienda moja kwa moja nyavuni, ukimzidi ujanja kipa David de Gea.

Bao la winga huyo wa Kibrazili liliifanya Betis kuongoza kwa mabao mawili, huku akiwa amechangia bao la 10 kwa miamba hiyo ya La Liga tangu alipojiunga kwa mkopo akitokea Man United kwenye dirisha la Januari.

Luca Ranieri aliifungia bao Fiorentina na kuwapa matumaini kwenye mechi ya marudiano itakayofanyika Italia. Antony amekuwa na maisha mazuri huko Seville na Man United ilikataa ofa ya Pauni 25 milioni ya kumtoa kwa mkopo mwingine mchezaji huyo msimu ujao, lakini imefungua milango ya kumuuza jumla.

Lakini, gwiji wa Betis, Joaquin ameitaka timu yake hiyo ya zamani kufanya kila inachokiweza ili Antony, 25, abaki.

Joaquin, 43, kwa utani alisema: "Nitatoa gari kama itahitajika kutekwa, lakini abakizwe kwa nguvu zote. Huu ni muda wa kufurahia, nadhani mambo matamu zaidi yatakuja, ngoja tuone."

Bao la Antony lilikuwa la sita kwa upande wake huku akiwa ameasisti mara nne pia katika mechi 19 alizochezea kikosi hicho kinachonolewa na Manuel Pellegrini tangu alipojiunga Januari.