He! avunja ukimya

NEPLE, ITALIA. STRAIKA wa Napoi Victor Osimhen amevunja ukimya baada ya kubezwa kupitia akaunti ya TikTok ya Napoli mwezi uliopita.
Hatua hiyo imekuja baada ya kukosa penalti katika mechi ya Serie A dhidi ya Bologna mwezi uliopita na kuzua gumzo mtandaoni, Napoli ikiambulia sare ya 0-0.
Wakala wa staa huyo, Roberto Calenda, alithibitisha wazi Osimhen alipanga kuichukulia hatua dhidi ya kufuatia kitendo hicho.
Calenda aliandika kupitia akauntiya X: "Kilichotokea kwenye akaunti ya TikTok ya Napoli haikubaliki, Ukweli ni kwamba imemuathiri mchezaji, wamemuongezea matatizo kwani bado ana mgogoro na waandishi wa habari kuhusu taarifa feki kuhusu yeye. Tunataka haki ifuate mkondo wake."
Sasa nyota huyo wa kimataifa wa Nigeria amefunguka kwa kusema: "Kuja katika mji wa Napoli mwaka 2020 yalikuwa maamuzi mazuri kwangu. Watu wa Napoli walinionyesha upendo wa hali ya juu, na sitakubali watu kuweka dosari kati yetu. Upendo wa watu wa Napoli umenifanya kucheza kwa bidii kutoka moyoni ndio maana navaa jezi kwa kujivunia. "Kashfa dhidi ya watu wa Napoli si kweli. Nina marafiki wengi kutoka Napoli wamekuwa sehemu ya familia yangu na maisha ya kila siku. Ninawashukuru nguzu zangu kutoka Nigeria kwa sapoti na kutoa sauti kwa ajili ya kuniunga mkono."
Osimhen, 24, alizungumza kutokana na mashabiki kuijia juu klabu ya Napoli walipombeza kupitia video kwa kutumia sauti ya kushangaza.
Hata hivyo traika huyo aligoma kupiga penalti dhidi ya Udinese wiki iliyopita na kuanzia benchi wikiendi iliyopita dhidi ya Lecce katika mechi ya Serie A.
Osimhen amekubali sakata hilo kumalizwa huku mtendaji mkuu anayedili na mambo ya mitandao ya kijamii ya klabu Alessio Fortino akijiuzulu nafasi yake.