Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haya mzigo wa Tuchel huo hapo England

Muktasari:

  • Timu ya taifa ya soka ya England, Three Lions imepangwa kwenye Kundi K katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026 sambamba na timu za Serbia, Albania, Latvia na Andorra. Kocha huyo Mjerumani, ambaye ataanza kazi ya kuinoa England, Januari mwakani, lakini mechi yake ya kwanza itakuwa Machi.

LONDON, ENGLAND: KOCHA, Thomas Tuchel sasa ameshafahamu mechi zake za kwanza kwenye kibarua chake cha timu ya taifa ya England atakabiliana na timu ipi na kwenye michuano gani.

Timu ya taifa ya soka ya England, Three Lions imepangwa kwenye Kundi K katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026 sambamba na timu za Serbia, Albania, Latvia na Andorra. Kocha huyo Mjerumani, ambaye ataanza kazi ya kuinoa England, Januari mwakani, lakini mechi yake ya kwanza itakuwa Machi.

Mechi ya kwanza ya Tuchel kwenye kikosi cha England itakuwa uwanjani Wembeley dhidi ya Albania, Machi 21 mwakani kwenye michuano hiyo ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 kwa mataifa ya Ulaya.

Siku tatu baadaye, kutakuwa mechi nyingine ambapo Three Lions itakipiga na Latvia. Mchezo wake wa tatu utakuwa Juni 7, ugenini Andorra.

Baada ya hapo itafuata mechi ya kirafiki na mpinzani ambaye bado hajafahamika.

Mechi ya marudiano dhidi ya Andorra itapigwa Septemba 6 na siku tatu baadaye England itakipiga na Serbia.

Kwenye mchakamchaka huo wa mechi za kufuzu, mechi nyingine ya Latvia itakuwa Oktoba 14, Serbia itakuwa Novemba 13 na Albania itakuwa Novemba 16. Kutakuwa na mechi ya kirafiki kabla ya kuikabili Latvia, Oktoba 14.

Tuchel alifichua kwamba ataanza upya kabisa kwenye kikosi hicho cha England, ikiwamo kuzungumza na wachezaji ambao awali waligoma kuitumikia Three Lions, akiwamo beki wa Arsenal, Ben White.