Hawa wakikuacha huwakuti kwa spidi

LONDON, ENGLAND. WINGA wa Chelsea, Mykhaylo Mudryk alisifiwa kuwa miongoni wa wachezaji wenye kasi zaidi duniani alipojiunga katika dirisha dogo la usajili la Januari lililopita.
Lakini winga huyo wa kimataifa wa Ukraine ameshindwa kuvunja rekodi ya beki wa Manchester City, Kyle Walker kwani ndio anaongoza katika orodha ya wachezaji wenye spindi wa Ligi Kuu England msimu huu. Katika orodha hiyo ya wachezaji wenye spidi kali wametenganishwa kwa tofauti ya kilometa 1.24 kwa saa.
Hii inakuwa msimu wa pili mfululizo kwa beki kuongoza katika orodha, msimu uliopita Antonio Rudiger ndiye alikuwa anaongoza wakati anakipiga Chelsea.

Hawa hapa wachezaji watano wenye spidi kali wa Ligi Kuu Engaland msimu huu akiwemo mfungaji bora Erling Haaland.


Kyle Walker (Manchester City) - Kilometa 37.31
Wlaker ndiye mchezaji anayeajwa kuwa beki bora kushoto wa Lig Kuu England, beki huyu alikuwa na mchango mkubwa Mancester City ikiibuka kuwa bingwa wa msimu huu. Walker alipambana hadi akaipata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza. Licha ya kuwa na umri wa amiaka 33 bado kiwango chake kimeendelea kuimarika zaidi. Walker anajiandaa kucheza fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester United kesho kutwa.


Brennan Johnson (Nottingham Forest) - Kilometa 36.70
JOHNSON alikiwasha msimu huu na kuisaidia Nottingham Forest ishuke daraja msimu huu. Alionyesha kiwango bora na kuwavutia mashabiki msimu huu. Ndio mchezaji pekee aliyecheza mechi 38 katika mashindano yote msimu huu. Mabao aliyofunga ni manane msimu huu. Straika huyu alikuwa mwiba katika safu ya ulinzi wa timu pinzani kutokana kasi yake msimu huu. Uwezo wake wa kukimbia kwa spidi ya 36.70.


Mykhaylo Mudryk (Chelsea) - Kilometa 36.63
WINGA huyu ndio anaongoza kuwa na spidi kwenye kikosi cha The Blues msimu huu. Mudryk alijiunga katika dirisha dogo la usajili kwa Pauni 89 milioni akitokea Shakhtar Dontesk. The Blues iliipikua n Arsenal kwenye uhamisho, ingawa hakung'ara licha ya kununuliwa kwa mkwanja mrefu. Hata hivyo Mudryk alijitahidi kukionyesha kiwango chake Stamford Bridge ndani ya miezi sita aliyocheza tangu alipotua. Winga huyo anaiingia katika orodha hii akiw mchezaji wa tatu mwenye spidi Ligi Kuu England.


Anthony Gordon (Newcastle) - Kilometa 36.61
NEWCASTLE ilitumia pesa ndefu ilipomsajili Anthony Gordon kutokea Everton katika dirisha dogo la usajili la kiangazi. Hata hivyo Gordon aliyumba msimu huu kwani amefunga bao moja tu katika mechi 16 alizocheza. Gordon alicheza nusu ya pili ya msimu na akaisaidia Newcastle kufuzu michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya msimu ujao. Katika orodha ameshika nafasi ya nne ya mchezaji mwenye spidi. Amekimbia kwa spidi ya kilometa 36.61.


Darwin Nunez (Liverpool) - Kilometa 36.53
DARWIN Nunez alitarajiwa angefanya mambo makubwa baada ya kusajiliwa kwa rekodi ya usajili dirisha la usajili la kiangazi lililopita. Hata hivyo straika huyo akashindwa kufikia malengo. Kuna matumaini ya kwamba Nunez atakuwa moto wa kuotea mbali msmu ujao. Licha ya kuzingua msimu huu anashika nafasi ya nne katika orodha ya wachezaji wenye spidi.


Arnaut Danjuma (Tottenham) - Kilometa 36.34
DANJUMA alisajiliwa dirisha dogo la usajili Januari, mashabiki waliusifia usajili huu lakini akashindwa kutoboa. Winga huyo alianza kikosi cha kwanza mara moja tu. Lakini bado ameshikilia rekodi ya kuwa mchezaji mwenye spidi Ligi Kuu England msimu huu uliomalizika. Danjuma amecheza mechi nane tu na alikuwepo katika kikosi cha Spurs kilichochezea kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Brentfotd


Matheus Nunes (Wolves) - Kilometa 36.32
NUNEZ alihusishwa na Liverpool lakini baadaye akajiunga na Wolves. Kiungo huyo alionyesha ubora wake msimu huu kutokana na spidi yake. Aliweka rekodi ya kukimbia kwa spidi ya kilometa 36.32 msimu huu. Nunez alikuwa na mchango akaisaidia Wolves kuepuka kushuka draja msimu huu.


Erling Haaland (Manchester City) - Kilometa 36.22
HAALAND amemaliza msimu kwa mafanikio makubwa, timu yake imeibuka kuwa bingwa wa Ligi Kuu England. Straika huyo aliweka rekodi kali ndnai ya msimu wake wa kwanza. Amefunga mabao 36 katika mechi 35 alizocheza kwenye ligi. Haaland atacheza fainali mbiliya kwanza Kombe la FA dhidi ya Manchester United, na fainali ya pili itakuwa ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Inter Milan.