Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hatima ya Ubingwa La Liga, vita ya nne bora na msukosuko wa kushuka daraja

BARCA Pict

Muktasari:

  • Barca wanasafiri kwenda Pamplona bila Lamine Yamal, ingawa Raphinha na Marc Bernal wanaweza kucheza. Osasuna, walio katika nafasi ya tisa na wakisaka nafasi za kucheza mashinda ya klabu Ulaya, watamkosa winga Victor Munoz ambaye ameripotiwa kuzivutia klabu zote mbili Barcelona na Real Madrid, lakini yuko nje kutokana na jeraha la mguu.

MADRID, HISPANIA: MZUNGUKO wa 34 wa Ligi Kuu Hispania, La Liga unaopigwa mwishoni mwa wiki hii unaweza kushuhudia ubingwa ukiamuliwa kwa kiasi kikubwa na nafasi nyingine ya Ligi ya Mabingwa kuthibitishwa, ambapo Barcelona watatangazwa mabingwa iwapo watashinda ugenini dhidi ya Osasuna, leo Jumamosi na Real Madrid wakipoteza dhidi ya Espanyo, kesho Jumapili.

Barca wanasafiri kwenda Pamplona bila Lamine Yamal, ingawa Raphinha na Marc Bernal wanaweza kucheza. Osasuna, walio katika nafasi ya tisa na wakisaka nafasi za kucheza mashinda ya klabu Ulaya, watamkosa winga Victor Munoz ambaye ameripotiwa kuzivutia klabu zote mbili Barcelona na Real Madrid, lakini yuko nje kutokana na jeraha la mguu.

Espanyol kwa upande wao wanawakaribisha Real Madrid baada ya suluhu nyumbani dhidi ya Levante waliopo nafasi ya pili kutoka mkiani, hali iliyoifanya klabu hiyo kuendeleza rekodi ya bila ushindi mwaka huu, na kushuka kutoka kwenye mbio za Ulaya hadi nafasi ya 13, pointi tano tu juu ya mstari wa kushuka daraja.

BARC 01

Nao Real Madrid watamkosa beki Eder Militao, ambaye amefanyiwa upasuaji wa kano na atakosa Kombe la Dunia, huku Arda Guler na Kylian Mbappe wakiwa nje kutokana na matatizo ya misuli. Kwa kuwa ubingwa uko karibu kutoka mikononi, kuna hisia kuwa baadhi ya wachezaji wanapendelea kubaki fiti kwa ajili ya majira ya kiangazi ya Kombe la Dunia 2026.

Iwapo ubingwa hautaamuliwa mwishoni mwa wiki hii, uwezekano mkubwa wa kuamua utakuwa katika mechi ya El Clasico kati ya Barcelona na Real Madrid itakayopigwa Mei 10.

BARC 02

Mchezo meingine Villarreal wanawakaribisha Levante, leo Jumamosi, katika mechi yenye athari pande zote mbili za msimamo. Sare kwa Villarreal walio nafasi ya tatu itawahakikisha kimahesabu kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku ushindi ukiweza kuwainua Levante wanaosafiri umbali mfupi kutoka Valencia, kutoka kwenye nafasi tatu za mwisho.

Villarreal pia watahakikisha kumaliza katika nne bora iwapo Real Betis watashindwa kuwafunga Real Oviedo waliopo mkiani, ambao matumaini yao ya kubaki Ligi Kuu Hispania yameathiriwa na kipigo cha nyumbani cha mabao 2-1 dhidi ya Elche mwishoni mwa wiki iliyopita.

BARC 03

Mzunguko huu wa mechi za LaLiga ulianza jana, Ijumaa usiku kwa Girona ikiwa nyumbani dhidi ya Mallorca katika mechi muhimu ya kuepuka kushuka daraja, ambapo iwapo ilipokea kipigo kinaweza kuivuta Real Mallorca kurudi katika nafasi tatu za mwisho.

Kwa upande wao Valencia wanaweza kuwa karibu kuondoa hofu ya kushuka daraja kwa ushindi wa nyumbani dhidi ya Atletico Madrid, ambao kocha wao Diego Simeone anatarajiwa kuwapumzisha wachezaji wake wengi wa kikosi cha kwanza kabla ya mechi ya marudiano ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal, inayotarajiwa kupigwa Jumanne kufuatia sare ya baoa 1-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Madrid, Jumatano iliyopita.

BARC 04

Nao Alaves wanawakaribisha Athletic Club katika Dabi ya Basque, huku Alaves wakihitaji sana pointi tatu na wakitumaini mshambuliaji mwenye kiwango bora Toni Martinez ataongeza mfululizo wake wa kufunga.

Athletic, ambao bado hawajawa salama kimahesabu, watalazimika kuendana na nguvu ya Alaves katika uwanja uliojaa wa Mendizorroza. Hayo yakiendelea, ushindi wa kwanza wa ugenini wa Elche msimu huu mwishoni mwa wiki iliyopita uliwaondoa katika eneo la kushuka daraja kabla ya kuifuata Celta Vigo ambayo bado iko nafasi ya saba licha ya kupoteza mechi tatu mfululizo.

BARC 05

Getafe, kwa upande mwingine, watajaribu kurejea baada ya kipigo dhaifu dhidi ya Barcelona watakapokutana na Rayo Vallecano ambao wana jicho moja kwenye nusu fainali ya Conference League dhidi ya Strasbourg ya Ufaransa wiki ijayo.

Nao Sevilla wanafunga mzunguko huo nyumbani dhidi ya Real Sociedad, keshokutwa Jumatatu, wakianza mechi wakiwa ndani ya eneo la kushuka daraja huku mvutano ukiongezeka ndani na nje ya uwanja.

Jambo moja chanya kwa kikosi cha kocha Luis Garcia Plaza ni kwamba Real Sociedad tayari wameshajihakikishia kucheza Europa League msimu ujao kwa kushinda Copa del Rey na hawana mengi ya kupigania zaidi ya heshima.