Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hali ilivyo Manchester City

Man City Pict

Muktasari:

  • Sare ya katikati ya wiki iliyopita dhidi ya Brentford kwenye Ligi Kuu England ilikifanya kikosi hicho cha Pep Guardiola kushuka hadi nafasi ya sita kwenye msimamo baada ya mechi 21.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER City bado inakwenda mwendo wa kobe kwenye Ligi Kuu England, lakini kinachosemwa wanataka kulitumia dirisha hili la Januari kuboresha kikosi chao kijanja ili kukifanya kirudi kwenye makali yake ya kutisha.

Sare ya katikati ya wiki iliyopita dhidi ya Brentford kwenye Ligi Kuu England ilikifanya kikosi hicho cha Pep Guardiola kushuka hadi nafasi ya sita kwenye msimamo baada ya mechi 21.

Kabla ya mechi za jana Jumamosi, ilikuwa imeanza pointi tatu kuifikia Newcastle United kwenye nafasi ya nne, lakini ilikuwa imeachwa nyuma kwa pointi 12 dhidi ya vinara Liverpool, ambao pia bado wana mechi moja mkononi.

Man City imeshaonyesha imeanza kujinasua kabla hata ya kufanya usajili wao wa kwanza kwenye dirisha hili la Januari. Kinara wao wa mabao, Erling Haaland amesaini mkataba mpya ambao unamfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa kuzidi ya wote kwenye Ligi Kuu England.

Bado kikosi kina wachezaji kadhaa majeruhi, akiwamo kiungo Rodri ambaye huenda akakosekana kwa msimu wote huku mabeki John Stones na Ruben Dias nao wamekosekana kwenye mechi za karibuni. Hata hivyo, usajili wa mastaa wanne wapya unaweza kubadili hali ya mambo kwenye kikosi cha Man City.

Nguvu yao kubwa kwenye usajili katika dirisha hili, Man City imeielekeza kwenye safu ya ulinzi. Abdukodir Khusanov anajiandaa kutua Etihad akitokea Lens, huku beki wa kati mwenzake Vitor Reis yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wake wa Pauni 29.5 milioni kutoka Palmeiras.

Kwenye fowadi, kikosi hicho cha Guardiola kinatarajia kurejea na ofa iliyoboreshwa kwenye usajili wa Omar Marmoush, licha ya kwamba si wao tu miamba ya Ligi Kuu England inayohitaji huduma ya mkali huyo wa Eintracht Frankfurt.

Mchezaji wa nne ambaye Man City inaweza kumnasa kwenye dirisha hili la Januari ni beki wa pembeni, Andrea Cambiaso kutoka Juventus. Na kama dili hizo nne zitafanyika, basi Man City itakuwa na kikosi tofauti kabisa wakati dirisha la Januari litakapofungwa na Guardiola anaweza kuwa na kikosi kitakachobadili hali ya mambo na kurudi kibabe uwanjani.

Kipa na safu ya ulinzi; Man City inaweza kukamilisha dirisha hili la Januari kwa kusajili mabeki wawili wa kati, lakini hilo halina maana kwamba wote wataanza kwenye kikosi cha kwanza kwa maana ya kuwa na pacha mpya kwenye beki ya kati.

Beki wa kimataifa wa Uzbek, Khusanov ana nafasi kubwa ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza na kinda Reis atasubiri kwa sababu bado hana uzoefu na soka la Ulaya.

Kama dili la Cambiaso litakamilika, hilo litawafanya Man City kumtumia Josko Gvardiol kwenye beki ya kati. Gvardiola amekuwa akifanya vizuri pembeni, lakini hilo haliifanyi Man City kupuuza kilichowafanya wavunje beki kunasa huduma yake baada ya kuvutiwa kwa kucheza beki wa kati RB Leipzig.

Kutokana na Kyle Walker kupiga hesabu za kuondoka hilo litamfanya Manuel Akanji aondoke kwenye beki ya kati na kucheza pembeni kulia akisaidiana na Rico Lewis. Golini ataendelea kubaki Ederson na msaidizi wake Stefan Ortega.

Kiungo; Rodri yupo nje kwa msimu mzima, licha ya kwamba chochote kinaweza kutokea na Mhispaniola huyo akarudi uwanjani kabla ya msimu kumalizika.

Kwa sasa kocha Guardiola anatafuta namna mpya ya kucheza soka lake kwenye safu ya kiungo. Kwa kipindi hiki, viungo Mateo Kovacic amekuwa akitumika kwenye eneo hilo la katikati ya uwanja, sambamba na Kevin De Bruyne na Bernardo Silva, wakipambana kwenye safu ya viungo watatu.

Fowadi; Mpango wa usajili kwenye dirisha hili la Januari kwenye kikosi cha Man City unamlenga pia fowadi wa Frankfurt, Marmoush, lakini atakapotua Etihad anaweza kutumika pia kama winga.

Hilo halitakuwa jambo la kushangaza chini ya Guardiola, kwa sababu hata Julian Alvarez alikuwa akitumika pembeni licha ya kuwa mshambuliaji wa kati kabla ya kutimkia zake Atletico Madrid wakati wa dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana.

Savinho amekuwa akifanya vizuri tangu alipotua Etihad akitokea Troyes, lakini kwenye nafasi mbili zilizobaki kwenye fowadi, Guardiola bila shaka ataanza na Phil Foden na Haaland, huku Jeremy Doku na Jack Grealish wakiwa ni machaguo mengine ya upande wa pembeni bila ya kumsahau Oscar Bobb.