Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gyokeres, Osimhen kung’oa wachezaji 11 Chelsea

TETESI Pict

Muktasari:

  • Licha ya kufanya usajili wa mastaa mbalimbali kwa miaka miwili, Chelsea bado inasumbuka kupata mtu sahihi kwenye safu yake ya ushambuliaji na imepanga kufanya maboresho ya eneo hilo msimu utakapomalizika.

CHELSEA huenda ikauza hadi wachezaji 11 katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu ikiwa ni pamoja na wachezaji wawili wa England, mshambuliaji Raheem Sterling, 30, na beki mwenye umri wa miaka 28, Ben Chilwell ili kupata pesa ambazo zitawasaidia kufanya maboresho kwenye eneo lao la ushambuliaji.

Licha ya kufanya usajili wa mastaa mbalimbali kwa miaka miwili, Chelsea bado inasumbuka kupata mtu sahihi kwenye safu yake ya ushambuliaji na imepanga kufanya maboresho ya eneo hilo msimu utakapomalizika.

Hata hivyo, italazimika kuuza kwanza ili kuepukana na sheria za matumizi ya pesa kwa sababu zimeshatumia kiasi kikubwa cha pesa katika sajili nyingi kwa miaka miwili.

Miongoni mwa washambuliaji ambao Chelsea inahusishwa nao kwamba inaweza kuwasajili katika dirisha lijalo ni pamoja na Victor Osimhen na Viktor Gyokeres.


Angel Gomes

KIUNGO wa Lille na England, Angel Gomes, 24, amekataa ofa ya mshahara wa Pauni 100,000 kwa wiki kutoka West Ham, inayohitaji huduma yake kwa msimu ujao.

Gomes ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu, anaripotiwa kukataa ofa hiyo kwa sababu anahitaji kujiunga na timu itakayokuwa inashiriki michuano ya kimataifa.


Benjamin Sesko

ARSENAL inataka kusajili straika atakayeirejesha kwenye kupigania makombe na imeweka macho yake kwa Alexander Isak, 25, Benjamin Sesko, 21, na Victor Gyokeres. Kwa kuwa bei ya Isak ya Pauni 130 milioni inaweza kuwatoa mchezoni, Arsenal inaweka nguvu katika kumsajili Sesko kutoka RB Leipzig ambaye anauzwa kwa Pauni 66 milioni na ana rekodi ya kuzifunga timu kubwa nyingi msimu huu -- Bayern Munich, Juventus, Atletico Madrid na Borussia Dortmund. Pia Sesko ni mrefu kuliko wawili hao wengine na umri wake ni mdogo zaidi yao.


Antony

WAWAKILISHI wa Real Betis watakutana na Manchester United kujadili mustakabali wa winga raia wa Brazil, Antony, 25, ambaye ameonyesha uwezo mkubwa tangu ajiunge nao kwa mkopo msimu huu. Antony ambaye hakuwa sehemu ya mipango ya kocha Ruben Amorim anaonekana kuwa mmoja kati ya mastaa tegemeo wa Betis kiasi cha timu hiyo kutaka kumpa mkataba wa kudumu.


Julian Alvarez

MABOSI wa Atletico Madrid wamesisitiza kwamba mshambuliaji wao wa kimataifa wa Argentina, Julian Alvarez, 25, hauzwi katika dirisha lijalo licha ya tetesi zinazozidai kwamba anaweza kusajiliwa na Liverpool kwa ajili ya kuziba pengo la Mohamed Salah ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu. Mkataba wa sasa wa Alvarez unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.


Noni Madueke

WINGA wa Chelsea na England, Noni Madueke, 23, yupo katika rada za AC Milan ambayo inahitaji kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Madueke ambaye mkataba wake na Chelsea unamalizika mwaka 2030, anatamani kuachana na timu hiyo kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza.


Raul Asencio

BEKI wa Real Madrid na Hispania, Raul Asencio, 22, anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika viunga vya timu hiyo kwa muda mrefu zaidi.

Mkataba wa sasa wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwakani.

Msimu huu amecheza mechi 40 za michuano yote.


Junior Firpo

REAL Betis ni kati ya timu zinazohitaji saini ya beki wa kushoto wa Leeds na Jamhuri ya Dominika, Junior Firpo, 28, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Mabosi wa Betis wameshawishika na mpango wa kutaka kumsajili nyota huyu kwa sababu mkataba wake utakuwa unamalizika mwisho wa msimu huu, hivyo itampata bure.