Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gyokeres ajifananisha na Haaland, Kane EPL

GYOKERES Pict

Muktasari:

  • Hilo linakuja wakati huu staa huyo wa kimataifa wa Sweden akidaiwa kukaribia kabisa kutua kwenye kikosi cha Arsenal, huku akidai kwanza ana hasira na Ligi Kuu England.

LONDON, ENGLAND: WANASEMA kama hupaishwi, jipaishe mwenyewe. Ndicho anachokifanya straika, Viktor Gyokeres, baada ya kudai kwamba yeye ni mkali kama ilivyo kwa Erling Haaland na Harry Kane ndani ya uwanja.

Hilo linakuja wakati huu staa huyo wa kimataifa wa Sweden akidaiwa kukaribia kabisa kutua kwenye kikosi cha Arsenal, huku akidai kwanza ana hasira na Ligi Kuu England.

Gyokeres, 27, yupo kwenye mipango yake ya kwenda kulipa kisasi Ligi Kuu England baada ya kushindwa kufanya hivyo alipokipiga kwenye ligi hiyo na sasa anataka kufanikisha usajili wake kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi, ili akawaonyeshe mabeki kile anachoweza kufanya.

Alipoulizwa kama yupo kwenye viwango vya Kane na Haaland, alisema: “Ndiyo, mimi ni mmoja wao.

GYO 01

"Nipo kwenye meza moja na hao jamaa. Nilichoweza kukifanya Sporting, nina hakika nitakwenda kukifanya kila mahali. Bado hamjaona ubora wangu.”

Staa huyo anataka kujiunga na Arsenal tu kwenye dirisha hili licha ya Manchester United, iliyojaribu mchakato wa kumsajili straika huyo pia. Staa huyo alishindwa kucheza mechi yoyote ya Ligi Kuu England kwa kipindi cha miaka mitatu aliyokuwa Brighton, kisha alikwenda kuwa na misimu miwili mizuri huko Coventry. Na kuhusu Ligi Kuu England, Gyokeres alisema: “Ni moja ya ligi kubwa Ulaya.

“Nilitumikia miaka kadhaa pale bila ya kucheza mechi hata moja. Hivyo, ni kitu ninachotaka kwenda kukifanya. Kitakwenda kuwa kisasi kizuri.”

GYO 02

Kuhusu ishu ya ubora wake kulingana na wakali Kane na Haaland, takwimu za Gyokeres kwa msimu uliopita zinapiga kelele juu ya jambo hilo.


MAVITU YA GYOKERES HUKO SPORTING 2024-25

-Amecheza: Mechi 52

-Amefunga: Mabao 54

-Ametoa: Asisti 13

-Uwanjani: Dakika 4,248

-Kazi za njano: 6

-Kadi nyekundu: 0

-Mataji: 2


MAVITU YA KANE

BAYERN 2024-25

-Amecheza: Mechi 41

-Amefunga: Mabao 41

-Ametoa: Asisti 14

-Uwanja: Dakika 3,958

-Kazi za njano: 7

-Kadi nyekundu: 0

-Mataji: 1


MAVITU YA HAALAND

MAN CITY 2024-25

-Amecheza: Mechi 48

-Amefunga: Mabao 34

-Ametoa: Asisti 5

-Uwanja: Dakika 4,041

-Kazi za njano: 2

-Kadi nyekundu: 0

-Mataji: 0