Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gyokeres ahofia dili la Arsenal kuvunjika

Muktasari:

  • Fowadi huyo wa kimataifa wa Sweden ameweka wazi dhamira yake ya kwenda kujiunga na The Gunners kwenye dirisha hili, huku akiwa hana mpango kabisa wa kubaki Sporting.

LONDON, ENGLAND: STRAIKA Viktor Gyokeres atafikiria uamuzi wa mkopo kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi endapo kama Sporting na Arsenal zitashindwa kufikia makubaliano juu ya ada ya uhamisho.

Fowadi huyo wa kimataifa wa Sweden ameweka wazi dhamira yake ya kwenda kujiunga na The Gunners kwenye dirisha hili, huku akiwa hana mpango kabisa wa kubaki Sporting.

Manchester United ilikuwa kwenye mchakato wa kumsajili straika huyo, lakini sasa Arsenal wanaonekana kuwa wenye nafasi nzuri ya kunasa saini yake.

Mkurugenzi wa michezo wa Arsenal, Andrea Berta alisafiri kwenda Ureno kukamilisha dili hilo, lakini ripoti zinafichua kwamba bosi huyo ameshaondoka Lisbon, lakini makubaliano baina ya klabu hizo mbili yakiwa hayajafikiwa. Na kinachoelezwa ni kwamba ni Arsenal wanaotaka kusitisha mazungumzo na kujiondoa kwenye hilo, kutokana na Sporting inavyomthaminisha Gyokeres.

Na sasa, straika Gyokeres na wawakilisha wake kwa sasa wameanza kupata wasiwasi kwamba dili hilo pengine likashindwa kukamilika. Kama mambo yatakwama, basi atafikiria uhamisho wa mkopo kwenda kujiunga na klabu nyingine ya Ulaya kwa sababu tu hataki kuendelea kuichezea Sporting.

Hilo ni kama lililotokea kwa straika Victor Osimhen kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana wakati timu yake ya Napoli iliposhindwa kumpiga bei, ambapo aliamua kwenda zake Uturuki kujiunga na Galatasaray, ambako alikuwa moto kwelikweli msimu uliopita.

Ripoti zinafichua Fenerbahce ya kocha Jose Mourinho ni miongoni mwa timu zinazofukuzia huduma ya Gyokeres endapo kama atakuwa tayari kuhama kwa mkopo kwenye dirisha hili. Juventus nayo inafuatilia jambo hilo kwa ukaribu mkubwa.

Arsenal inataka Namba 9 mpya kwenye dirisha hili na ilikuwa na mpango wa kumchukua straika wa Red Bull Leipzig, Benjamin Sesko kabla ya kuhamia kwa Gyokeres, ambaye amefunga mabao 97 katika mechi 102 alizochezea Sporting tangu Agosti 2023.

Kinachoelezwa, Sporting inataka ilipwe Pauni 60 milioni kwanza, kisha Pauni 8 zitalipwa kama nyongeza. Makubaliano binafsi ya mchezaji na Arsenal yameshafikiwa, atasaini dili la miaka mitano.