Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gwiji wa soka asema Mbape hapati namba

Muktasari:

  • Ushamjua? Huyo huyo, Kylian Mbappe. Lakini, kuna gwiji mmoja, aliyewahi kushinda ubingwa wa Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Ufaransa, anasema tena kwa msisitizo kwamba fowadi huyo mpya wa Real Madrid, Mbappe hapati namba kwenye kikosi cha pamoja cha England na Ufaransa, ambacho zitaumana kwenye mikikimikiki ya Euro 2024 itakayoanza baadaye mwezi huu.

PARIS, UFARANSA: ANATAZAMWA kama mmoja wa wanasoka bora kabisa kwa sasa. Yupo kwenye kipindi cha kuelekea katika kilele cha soka lake na hivi karibuni amekamilisha uhamisho wa ndoto zake kwenye mchezo huo duniani.

Ushamjua? Huyo huyo, Kylian Mbappe. Lakini, kuna gwiji mmoja, aliyewahi kushinda ubingwa wa Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Ufaransa, anasema tena kwa msisitizo kwamba fowadi huyo mpya wa Real Madrid, Mbappe hapati namba kwenye kikosi cha pamoja cha England na Ufaransa, ambacho zitaumana kwenye mikikimikiki ya Euro 2024 itakayoanza baadaye mwezi huu.

Gwiji huyo ni Emmanuel Petit. Haijulikani kama ameamua kuwajaza tu England au anasema ukweli kutokana na uzoefu wake kwenye soka.

Kiungo huyo wa zamani wa Chelsea na Barcelona alipata nafasi ya kucheza na washambuliaji mahiri kabisa duniani wakiwamo Dennis Bergkamp na Thierry Henry, hivyo anaweza kuwa na mantiki anaposema kwamba kwenye upate wa washambuliaji, Mbappe huenda asipate nafasi mbele ya wakali wa England wanaounda safu yao ya ushambuliaji ambao watakuwapo kwenye Euro 2024 huko Ujerumani.

Petit anaamini safu ya washambuliaji watatu wa England ya sasa, wote wana ubora mkubwa wa kuanzishwa kwenye kikosi mbele ya Mbappe.

Nahodha wa Three Lion na kinara wa mabao wa timu hiyo, Harry Kane anajaribu kujiweka sawa kabla ya Euro 2024, huku ikifahamika wazi England na kikosi cha Les Bleus chini ya kocha Didier Deschamp zinaweza kukutana huko Ujerumani kwenye hatua ya nusu fainali.

Wakati huo Phil Foden amekuwa kwenye kiwango bora akitokea kuipa Manchester City taji la nne mfululizo la Ligi Kuu England. Na licha ya kwamba Bukayo Sako anadaiwa kiwango chake kinapanga na kushuka, lakini alikuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Arsenal na kufanikiwa ilichofanyikiwa kwenye Ligi Kuu England kwa msimu wa 2023-24.

Kwa ujumla wake, Petit anaamini kuna mastaa watano kwenye kikosi cha England cha sasa wanapata nafasi ya kuingia moja kwa moja kwenye timu ya Ufaransa, huku chama hilo la kocha Gareth Southgate likiwa miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa Euro 2024.

Mbappe alifunga hat-trick kwenye fainali ya Kombe la Dunia 2022 mbele ya Argentina, lakini hilo halikusaidia timu yake kubeba ubingwa huo.

Na Petiti anaamini kasi ya Mbappe uwanjani isingeweza kufua dafu mbele ya Saka au Foden kama mastaa hao wa England wangekuwa wanaweza kuchaguliwa kuichezea Ufaransa. Kwa maana hiyo Petit anachoamini ni kwamba Saka na Foden wanaweza kumweka benchi Mbappe.

Petit, 53, aliambia bestonlinepokersites.ltd: “Harry Kane angepata nafasi moja kwa moja kwenye timu ya Ufaransa kwa sababu anafunga mabao. Namheshimu Olivier Giroud, lakini Kane ameonyesha ni straika bora duniani kwa kipindi cha miaka 10 sasa.

“Hata kama tungekuwa na Mbappe kushoto na Ousmane Dembele kulia, hiyo haina maana kwamba Phil Foden asingeweza kuanza mbele ya Mbappe. Foden amekuwa na msimu bora sana. Amekuwa bosi wa Manchester City.

“Na upande mwingine, yupo Bukayo Saka, ambaye amekuwa kwenye kiwango bora sana kwa miaka minne iliyopita kwenye kikosi cha Arsenal.”

Petit hashangazwi na vipaji vilivyopo kwenye kikosi cha England ambao wana uwezo mkubwa wa kupata nafasi kwenye kikosi cha Les Bleus.

Petit, ambaye aliichezea Ufaransa mechi 64 alisema: “Nadhani kwenye eneo la kiungo kungekuwa na utawala mkubwa wa wachezaji wa England. Eneo hilo lina vipaji vikubwa sana. Jude Bellingham na Declan Rice wangeweza kucheza timu ya Ufaransa bila ya matatizo yoyote.”