Gundogan avunja rekodi ya Louis Saha, bao la mapema zaidi

LONDON, ENGLAND. Kiungo Ilkay Gundogan ameweka rekodi ya kufunga bao la mapema zaidi kwenye fainali ya Kombe la FA, akifunga sekunde ya 13 dhidi ya Man United akivunja rekodi ya Louis Saha wa Everton aliyefunga sekunde ya 25 kwenye fainali ya kombe hilo dhidi ya Chelsea 2009.

Man City wapewe maua yao msimu huu wamechukua Kombe la FA ikiichapa watani wao Manchester United mabao 2-1 katika uwanja wa Wambley huku IIkay Gundogan akiifungia akiitanguliazia Man City bao la mapema sana sekunde 13 na bao lingine dakika 51 kwa Man United bao limefungwa na Bruno Fernandes dakika ya 33.

Man City ya Pep Guardiola, yenyewe inafukuzia rekodi ya kihistoria ya kubeba mataji matatu makubwa ndani ya msimu mmoja, ili iifikie Man United ilipofanya hivyo chini ya Sir Alex Ferguson mwaka 1999.

Ikumbukwe hii ni fainali ya tisa Manchester United anapoteza Kwenye Kombe la FA

Siku zote, Manchester derby imekuwa na upinzani mkali ndani na nje ya uwanja, ambapo mashabiki wa kila timu watahitaji ushindi ili kuwatambia wenzao. Man United wamemaliza msimu wao leo, wakati Man City wao watasubiri kumaliza na Inter Milan huko Istanbul.

Man United imekamatia tiketi ya kucheza fainali ya Kombe la FA msimu huu baada ya kuwachapa Brighton kwa mikwaju ya penalti. Baada ya sare ya bila kufunga katika dakika 120, mikwaju ya penalti ilifuata na hapo Man United ikakamatia tiketi ya kwenda kucheza fainali na Man City, ambao wao kwenye nusu fainali walicheza na Sheffield United na kuwachapa 3-0, shukrani kwa mabao ya Riyad Mahrez, aliyefunga hat-trick siku hiyo.