Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola akubali maneno ya Mourinho

Muktasari:

  • Man City imecheza sehemu kubwa ya msimu huu bila ya huduma ya mshindi wa Ballon d’Or, Rodri na imekuwa ikikumbwa na majeraha kwa wachezaji wake muhimu, akiwamo mtambo wao wa mabao, straika Erling Haaland, ambaye atakosekana uwanjani kwa muda mrefu baada ya kuumia kwenye mechi iliyopita.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA, Pep Guardiola amesema kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya yatakuwa mafanikio makubwa kwenye kikosi cha Manchester City kutokana na majanga makubwa yanayowakabili msimu huu.

Man City imecheza sehemu kubwa ya msimu huu bila ya huduma ya mshindi wa Ballon d’Or, Rodri na imekuwa ikikumbwa na majeraha kwa wachezaji wake muhimu, akiwamo mtambo wao wa mabao, straika Erling Haaland, ambaye atakosekana uwanjani kwa muda mrefu baada ya kuumia kwenye mechi iliyopita.

Kocha huyo Mhispaniola alisema watu wanafanya makosa kuamini kwamba Man City kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ni uhakika kila msimu.

Jose Mourinho aliwahi kusema kumaliza nafasi ya pili nyuma ya Man City mwaka 2018 -- wakati anainoa Manchester United -- yalikuwa mafanikio yake makubwa zaidi katika kazi yake ya ukocha, wakati alipojaribu kuelezea pengo la ubora wa viwango lililokuwapo baina ya timu hizo mbili.

Guardiola inawezekana ameshinda mataji mengi sana akiwa na Man City, alisema, kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo itakuwa mara yao ya 15 mfululizo, yatakuwa mafanikio makubwa kwake upande wake.


“Kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao yatakuwa mafanikio makubwa, huo ndio ukweli kutokana na matatizo yanayotukabili,” alisema Guardiola.

“Naelewa sasa Jose aliposema haya maneno. Kwa timu hiyo, msimu ujao, tunataka kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya. Nilishasema hili kabla, mara milioni nadhani, kwamba watu wanachukulia uhakika Man City itafuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya kila msimu. Nafahamu jinsi ilivyokuwa ngumu. La sivyo, kila timu kubwa ingekuwa inafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kila msimu, lakini hilo halipo hivyo.”

Man City usiku wa Jumatano ilitarajia kukipiga na Leicester City na ilikuwa kwenye nafasi ya tano kwenye ligi, ikiwa ni pointi nne tu zimetofautisha na timu inayoshika nafasi ya 10 kwenye msimamo huo, Bournemouth, ambayo pia ipo kwenye vita kali ya kufukuzia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Guardiola alisema: “Tuna mechi tisa, fainali tisa na hizo tutazitumia kujaribu kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.”