Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guadiola anawaza Top Four tu basi

Muktasari:

  • Kocha huyo wa Man United amefichua kwamba kuna timu nyingi zimejaribu na kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini anaamini timu yake itarudi uwanjani kwa kasi kubwa baada ya kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Nottingham Forest, Jumamosi iliyopita.

MANCHESTER, ENGLAND: PEP Guardiola amekiri kushindwa kuwapo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao litakuwa ni tatizo, lakini hiyo haina maana kwamba ni mwisho wa makali ya Manchester City.

Kocha huyo wa Man United amefichua kwamba kuna timu nyingi zimejaribu na kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini anaamini timu yake itarudi uwanjani kwa kasi kubwa baada ya kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Nottingham Forest, Jumamosi iliyopita.

Guardiola alisema: "Kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya yatakuwa mafanikio makubwa sana, lakini ni lazima ushinde. Iwe upo kwenye nafasi ya tano, sita au saba kwenye msimamo, unahitaji kushinda. Nataka kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

"Itakuwa mbaya kama tutashindwa, lakini nimeona hilo likitokea mara nyingi kwenye timu nyingine za Ligi Kuu England huko nyuma. Kutokuwapo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya litakuwa ni tatizo, lakini timu ambazo zilishindwa kufuzu huko nyuma zimerudi kwa kishindo na sasa zinashiriki.

"Ni miaka mingapi Manchester City ilikuwapo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya hadi kufikia Februari? Miaka 10? Hapana, ni zaidi ya hilo. Na huko nyuma tulikuwa hatujawahi kuwapo kwenye michuano."

England inaweza kupata nafasi ya ziada kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kutokana na viwango vya Uefa. Lakini, hilo halimfanyi Guardiola kubweteka ambapo anapambana kuhakikisha kikosi chake kinamaliza ndani ya Top Four ili kukamatia tiketi hiyo.

Man City kwa sasa ipo nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, ambapo inaweza kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya kama mambo yatabaki kuwa hivyo na kuwapo kwa nafasi ya ziada, lakini Brighton, Aston Villa, Bournemouth na Newcastle United zenyewe pia zipo kwenye vita ya kuisaka nafasi hiyo.