Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Garnacho aingia anga za Napoli ikimpa njia ya kutokea

Tetesi Pict

Muktasari:

  • Conte anataka huduma ya fundi huyu wa kimataifa wa Argentina ili kuziba pengo la winga wao raia wa Georgia, Khvicha Kvaratskhelia ambaye ana uwezekano mkubwa wa kujiunga na  Paris St-Germain katika dirisha hili.

KOCHA wa Napoli, Antonio Conte amewasilisha jina la winga wa Manchester United, Alejandro Garnacho, 20, kwa mabosi wa timu hiyo ili asajiliwe katika dirisha hili.

Conte anataka huduma ya fundi huyu wa kimataifa wa Argentina ili kuziba pengo la winga wao raia wa Georgia, Khvicha Kvaratskhelia ambaye ana uwezekano mkubwa wa kujiunga na  Paris St-Germain katika dirisha hili.

Garnacho ni mmoja kati mastaa wa Man United walioingia katika sintofahamu na kocha mpya Ruben Amorim hali iliyosababishwa aachwe kwenye mchezo dhidi ya Arsenal kabla ya kurudishwa.

Inaelezwa, Amorim havutiwi na utendaji kazi wa Garnacho na Rashford ndio maana alifikia hatua ya kuwaondoa kwenye timu.

Napoli inaamini kuna asilimia nyingi za kumpata staa huyu kwa sababu ya kile kinachoendelea kati yake na kocha wa timu hiyo.

Mkataba wa sasa wa Gernacho unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Msimu huu amecheza mechi 30 za michuano yote na kufunga mabao nane.


Kyle Walker

BEKI kisiki wa Manchester City na England, Kyle Walker, 34, ana asilimia nyingi za kusaini mkataba wa miaka miwili na nusu kujiunga na AC Milan katika dirisha hili.

Kwa mujibu wa kocha wa Man City, Pep Guardiola beki huyu ameomba kuondoka katika dirisha hili.

Mbali ya Milan fundi huyu pia anahusishwa na timu kadhaa za Saudi Arabia ambako amewekewa ofa ya mshahara unaofikia Pauni 400,000 kwa wiki.



Ronald Araujo

INAELEZWA beki wa Barcelona na Uruguay, Ronald Araujo, anataka kuondoka timu hiyo katika dirisha na mpango wake ni kutua Juventus lakini Barcelona imeonyesha mpango wa kuzuia usajili wake ili kuendelea kumtumia kwenye kikosi chao ikiwa ni maelekezo ya kocha Hans Flick ambaye anaamini beki huyo wa kimataifa wa Uruguay anahitaji muda tu kurudi kwenye kiwango chake, kama alivyofunika juzi katika fainali ya Supercup ambayo Barca iliifunga Real Madrid 5-2.


Mats Hummels

BEKI kisiki raia wa Ujerumani, Mats Hummels, 36, hana presha ya kuanza mazungumzo ya mkataba mpya na AS Roma licha ya mkataba wake wa sasa kutarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.

Hummels ambaye kabla ya kujiunga na Roma aliwahi kuhitajika na timu za Marekani, msimu huu amecheza mechi 10 za michuano yote na kufunga bao moja.


Evan Ferguson

MSHAMBULIAJI wa Brighton na Jamhuri ya Ireland, Evan Ferguson, 20, pamoja na staa wa Manchester United na England, Marcus Rashford, 27, wanadaiwa kuwa katika hatua za mwisho kujiunga na West Ham kwa mkopo wa nusu msimu.

Inaelezwa mastaa hawa ni pendekezo la kocha mpya Graham Potter ambaye ameajiriwa mwezi huu baada ya kufukuzwa kwa Julen Lopetegui.


Harvey Elliott

BORUSSIA Dortmund imeanza mazungumzo na Liverpool kwa ajili ya kuipata saini ya kiungo wa timu hiyo na England, Harvey Elliott, 21, katika dirisha hili. Elliot amekuwa hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Liverpool tangu kuanza kwa msimu huu, hali inayosababisha ahitaji kuondoka katika dirisha hili. Dortmund inakumbana na upinzani mkali kutoka kwa Brighton.

Taarifa zinadai Bayern imempa ofa ya mshahara wa Euro 25 milioni kwa mwaka. Msimu huu amecheza mechi 22 za michuano yote.


Dominic Calvert-Lewin

ATALANTA inapambana kuhakikisha inakamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Everton na England,  Dominic Calvert-Lewin, katika dirisha hili licha ya upinzani mkali inaoupata kutoka kwa Newcastle United ambayo pia inahitaji huduma yake. Lewin ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu, anahusishwa pia na Como ya Italia.


Alphonso Davies

BAYERN Munich imempa ofa ya mkataba mpya beki wake raia wa Canada, Alphonso Davies, 24, ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.

Davies ambaye anayehusishwa sana na Real Madrid, ni miongoni mwa mastaa tegemeo wa wababe hao wa Ujerumani.

Taarifa zinadai Bayern imempa ofa ya mshahara wa Euro 25 milioni kwa mwaka. Msimu huu amecheza mechi 22 za michuano yote.