Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

GAME ON! Mbappe, Messi, Ronaldo walipofunga mabao 50 Ligi ya Mabingwa Ulaya

Mabao Pict

Muktasari:

  • Katika msimu huo, Mbappe akiwa kinda, alifunga bao kwenye raundi ya mtoano ya 16 bora, robo fainali na nusu fainali na kuwa na wastani wa kufunga mara moja katika kila baada ya dakika 89.3 katika michuano hiyo ya Ulaya kwa mwaka huo.

LONDON,ENGLAND: SUPASTAA, Kylian Mbappe hivi karibuni alifunga bao lake la 50 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Real Madrid ilipoichapa Atalanta, lakini imemchukua muda gani kufikia idadi hiyo ya mabao ukilinganisha masupastaa matata Lionel Messi na Cristiano Ronaldo?


Namba hazisemi uongo

Baada ya kuibukia kwenye mikikimikiki hiyo katika msimu wa 2016-17, Mbappe alionyesha kiwango bora sana katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakati alipofika hatua ya nusu fainali akiwa na kikosi cha AS Monaco.

Katika msimu huo, Mbappe akiwa kinda, alifunga bao kwenye raundi ya mtoano ya 16 bora, robo fainali na nusu fainali na kuwa na wastani wa kufunga mara moja katika kila baada ya dakika 89.3 katika michuano hiyo ya Ulaya kwa mwaka huo.

Kutokana na kiwango chake bora alichokionyesha akiwa na AS Monaco, hatimaye miamba ya soka ya Ufaransa, Paris Saint-Germain ilivutiwa naye na kwenda kunasa huduma yake kwa gharama ya Euro 180 milioni.

Katika kipindi chake cha miaka saba katika kikosi hicho cha Parc des Princess, Mbappe alionyesha kiwango bora kabisa na namba za kibabe kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, akifunga mabao 42 katika mechi 64 za michuano hiyo.

Hakuwahi kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na kikosi cha PSG, lakini alikaribia kufanya hivyo kwenye msimu wa 2019-20 wakati timu hiyo ilipofika fainali na kupoteza mbele ya wababe wa Ujerumani, Bayern Munich.

Tangu alipojiunga na Real Madrid, Mbappe amefunga mabao mawili kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya katika mechi sita alizotumikia Los Blancos, huku mabao hayo akifunga dhidi ya Stuttgart na Atalanta katika mtindo mpya wa michuano hiyo ya Ulaya unaotumika msimu huu.

Kwa ujumla wake, fowadi huyo Mfaransa, Mbappe alihitaji mechi 79 kufikisha mabao 50 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Lakini, je itamweka kwenye nafasi gani ukilinganisha na masupastaa wawili, Messi na Ronaldo?

Messi bao lake la 50 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya alifunga dhidi ya AC Milan, Aprili 2012, katika ushindi wa 3-1 kwenye mechi ya marudiano ya hatua ya robo fainali.

Kwenye mechi hiyo, Muargentina Messi alifunga mara mbili, hivyo akamaliza mechi hiyo akiwa na mabao 51. Hiyo ilikuwa mechi ya 66 kwake kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hivyo, ilimchukua Messi pungufu ya mechi 16 ukilinganisha na Mbappe kwenye kufikisha mabao 50 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo, kwenye kesi ya supastaa Ronaldo, ilimchukua mechi nyingi zaidi kufikisha idadi ya mabao 50 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ukilinganisha na wakali hao wawili, Messi na Mbappe.

CR7 alifikisha bao lake la 50 kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Aprili 2013, katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Borussia Dortmund.

Kwa ujumla, ilimchukua Mreno huyo mechi 91 kufikisha mabao 50 kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikiwa ni mechi 12 zaidi ya alizocheza Mbappe na mechi 25 zaidi ya alizocheza Messi.

Hata hivyo, wakati Ronaldo ikimchukua mechi nyingi kufikisha idadi ya mabao 50 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, alikuja kuwa moto wa kuotea mbali baadaye kwenye kutikisa nyavu katika michuano hiyo. Kwa mfano ilimchukua mechi 46 tu kufunga mabao 50 mengine kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, hiyo ina maana alihitaji mechi 137 kufikisha idadi ya mabao 100 kwenye michuano hiyo ya Ulaya.

Huu hapa mchanganuo ulivyo wa mastaa Mbappe, Messi na Ronaldo kwenye rekodi za mabao katika Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati walipofikisha mabao 50.