Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea FC yaipa utajiri Brighton

Muktasari:

  • Chelsea imeng’oa watu wasiopungua 14 wachezaji na mabosi kutoka Brighton, huku mtu wa mwisho kumtoa Amex ni straika Joao Pedro, aliyesajiliwa kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi kwa mkwanja wa Pauni 55 milioni.

LONDON, ENGLAND: HII kali. Chelsea imeilipa Brighton Pauni 257 milioni kwenye miaka ya karibuni, mkwanja ambao unatosha kujenga uwanja wake wa Amex mara tatu.

Chelsea imeng’oa watu wasiopungua 14 wachezaji na mabosi kutoka Brighton, huku mtu wa mwisho kumtoa Amex ni straika Joao Pedro, aliyesajiliwa kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi kwa mkwanja wa Pauni 55 milioni.

Makinda Zak Sturge na Shumaira Mheuka walikuwa wachezaji wa kwanza kuhama kwenye dirisha la majira ya kiangazi, ikiwa ni miezi michache baada ya Chelsea kuwa chini ya tajiri wa Kimarekani, Todd Boehly. Kisha akafuatia beki wa pembeni, Marc Cucurella kwa ada ya Pauni 62 milioni. Baadaye, Chelsea ilikwenda kumchukua kocha wa Brighton, Graham Potter.

Boehly alichukua uamuzi wa kumfuta kazi Thomas Tuchel wiki chache baada ya kuanza kwa msimu wa 2022-23 na hapo mikoba ilikabidhiwa kwa Potter, ambaye aliigharimu The Blues, Pauni 21 milioni kama fidia ya kuvunja mkataba wake huko Brighton. Potter alitua Stamford Bridge na wasaidizi wake watano, Billy Reid, Bjorn Hamberg, Bruno Saltor, Ben Roberts na Kyle Macauley.

Chelsea ilivamia tena Amex kwenda kunasa huduma ya Paul Winstanley, ambaye alikwenda kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa michezo na kwenye hilo, The Blues iliilipa tena fidia Brighton.

Mapema mwaka jana, Sam Jewell aliondoka Brighton kwenda Chelsea kuwa skauti wa miamba hiyo na kuhusika kwenye mazungumzo ya wachezaji. Kisha Chelsea ikavunja rekodi ya uhamisho Uingereza baada ya kumsajili kiungo Moises Caicedo kutoka Brighton kwa ada ya Pauni 115 milioni.

Ilifanya uhamisho pia wa kipa Robert Sanchez kwa ada ya Pauni 25 milioni nna sasa imefunga na usajili wa Joao Pedro kwenye dirisha hili, ikiifanya Brighton kuvunja mkwanja ambao kama itaamua kujenga viwanja vya aina ya Amex, basi itakuwa navyo vitatu.