Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gabriel Jesus afichua jambo Arsenal

GABRIEL Pict

Muktasari:

  • Mwezi uliopita, Rais wa klabu ya Palmeiras, Leila Pereira, alitoa maoni kuhusu fununu zilizodai kwamba Jesus anaweza kurejea timu hiyo anapoikaribia hatua ya mwisho ya kazi yake ya soka.

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Gabriel Jesus amefichua kuwa ndoto yake ni kurejea Palmeiras ya kwao Brazil.

Mwezi uliopita, Rais wa klabu ya Palmeiras, Leila Pereira, alitoa maoni kuhusu fununu zilizodai kwamba Jesus anaweza kurejea timu hiyo anapoikaribia hatua ya mwisho ya kazi yake ya soka.

“Bila shaka Gabriel Jesus. Na nitasema zaidi. Hivi karibuni utarudi nyumbani, Gabriel! Siku moja utarejea.”

Sasa, mshambuliaji huyo wa Arsenal alizungumza katika mahojiano na Revista Placar, akitafakari kuhusu uwezekano wa uhamisho ambao anasema hauna mantiki kwa sasa, lakini huenda ukatokea siku za usoni.

“Hakujawahi kuwa na mawasiliano na klabu nyingine. Tamaa yangu, kama ambavyo huenda nikawa nasema daima, ni kurejea Palmeiras. Na Palmeiras pia wanataka nirudi.”

“Wakati nitahisi kuwa ni wakati sahihi wa kurejea Palmeiras, nitaamua hilo pamoja na Arsenal.

“Lakini tunazungumza kuhusu mchezaji aliyekosa soka kwa miezi tisa na sasa anapambana kurejea kwenye timu. Baadhi ya waandishi wa habari huzungumza bila msingi wowote.”

“Baada ya upasuaji mgumu kiasi hiki, haina maana mimi kuondoka klabuni sasa.”

Jesus alikuwa akifanya mazoezi katika kituo cha Palmeiras wakati wa safari yake ya kupona na inasemekana ana utani wa mara kwa mara na wachezaji wenzake wa Brazil, Gabriel Magalhães na Gabriel Martinelli, kuhusu ushindani kati ya Palmeiras na Corinthians.

Mkataba wa Jesus unaisha mwaka 2027, jambo linalomaanisha Arsenal hawana shinikizo la kumuuza na anaporejea taratibu katika ubora wa kimwili, uamuzi utakuwa mikononi mwa kocha Mikel Arteta kama ataamua kumpa nafasi tena kikosini au kumruhusu kurejea nyumbani Brazil.