Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili jipya la Saka Emirates kufuru

Muktasari:

  • Kinachoelezwa ni kwamba dili hilo jipya linaweza kuwa na thamani ya Pauni 300,000 kwa wiki ili kuendelea kufanya mambo yake kwenye kikosi hicho cha Emirates.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL inaamini itashinda vita ya kumshawishi winga wao matata kabisa, Bukayo Saka juu ya kusaini dili jipya kwenye timu hiyo baada ya majadiliano ya muda mrefu.

Kinachoelezwa ni kwamba dili hilo jipya linaweza kuwa na thamani ya Pauni 300,000 kwa wiki ili kuendelea kufanya mambo yake kwenye kikosi hicho cha Emirates.

Mazungumzo na mawakala wa Saka yamefanyika kwa muda mrefu sasa na kinachoripotiwa ni kwamba pande zote mbili zipo kwenye makubaliano. Dili hilo jipya litamfanya Saka kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi huko Emirates.

Arsenal inaamini Saka atakwenda kuwa mmoja wa mawinga bora sana kwenye soka la Ulaya. Saka amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Arsenal, si tu kwa kiwango chake, bali kwa kile anachofanya akiwa ametokea kwenye akademia ya timu hiyo.

Arsenal inaamini Saka yupo kwenye nafasi kubwa ya kunyakua taji la Ligi Kuu England, hivyo hilo linaweza kumshawishi akasaini mkataba mpya na kubaki. Kiwango chake kwenye kikosi cha Arsenal kimemfanya Saka apate nafasi pia ya kujumuishwa kwenye timu ya England.

Mwezi uliopita, Saka alisema: "Nataka kuisaidia timu yangu kushinda mataji makubwa kwa kipindi nitakachokuwa Arsenal. Hivyo, hiyo ni hatua kubwa. Tuna vitu vingi vya kufanya kama timu kwa miaka mingi, licha ya kwamba tumepita kwenye mapito mengi tukiwa pamoja. Nataka kupiga hatua ya juu zaidi."

Wakati dili la Saka likikaribia kufikia mwafaka, mabosi wa Arsenal bado hawajaanza mazungumzo ya kumwongeza mkataba mpya kocha wao, Mikel Arteta.

Kocha huyo Mhispaniola yupo kwenye miezi 18 ya mwisho ya mkataba wake, lakini ishu ya kwamba anabaki au anaondoka bado haijawekwa kwenye mjadala.

Arteta alisubiri hadi mwaka wa mwisho wa mkataba wake uliopita kabla ya kusaini dili jipya na kuendelea kubaki kwenye kikosi cha Arsenal. Na pengine safari hii atahitaji kurudia hilo.

Arsenal kwa sasa inashika usukani wa Ligi Kuu England kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya Manchester City katika mbio za kusaka ubingwa.