Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FIFA yatangaza mashindano mapya Kusini-Mashariki mwa Asia

FIFA Pict

Muktasari:

  • Mashindano hayo yatakayofahamika kama Kombe la FIFA la ASEAN, yanakusudia kuimarisha maendeleo ya soka miongoni mwa watu takriban milioni 700 wa eneo hilo kupitia ushindani wa kimataifa ulio na mpangilio maalum.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, ametangaza kuanzishwa kwa mashindano mapya ya kandanda ya kanda yatakayohusisha nchi zote 11 za Kusini-Mashariki mwa Asia. 

Mashindano hayo yatakayofahamika kama Kombe la FIFA la ASEAN, yanakusudia kuimarisha maendeleo ya soka miongoni mwa watu takriban milioni 700 wa eneo hilo kupitia ushindani wa kimataifa ulio na mpangilio maalum.

Infantino ameeleza kuwa mashindano hayo yatatoa msukumo halisi katika ukuaji wa soka kwa kuwaleta pamoja wachezaji bora wa kanda hiyo, kwenye mfumo wa kimataifa ulio rasmi.

“Soka linaunganisha dunia, na pamoja na nchi zote 11 za ASEAN, tunaunda Kombe la FIFA la ASEAN, ninaamini mashindano haya yataleta umoja katika eneo hili kwa kuwa na mafanikio makubwa kwenye jukwaa la kimataifa la soka.” amesema rais huyo wa FIFA wakati wa akitoa tangazo kwenye mkutano maalum mjini Kuala Lumpur, Malaysia.

FIF 01

Tangazo hilo limetolewa na Rais wa FIFA kufuatia kutiwa saini kwa makubaliano ya ushirikiano kuhusu maendeleo ya soka ya kikanda wakati wa mkutano wa 47 wa Kilele wa ASEAN uliofanyika katika mji mkuu wa Malaysia. 

Infantino alisaini makubaliano hayo na Katibu Mkuu wa ASEAN, Kao Kim Hourn, huku Waziri Mkuu wa Malaysia, Anwar Ibrahim, akishuhudia kwa nafasi yake kama mwenyekiti wa ASEAN 2025. 

Makubaliano hayo yanaashiria dhamira ya FIFA ya kupanua maendeleo ya soka katika ukanda wa Kusini-Mashariki mwa Asia.

FIF 02

Wakati huo huo, Infantino ameeleza mkakati wa maendeleo wenye msingi wa nguzo tatu kuu, ambazo ni Kuhakikisha uadilifu na uwazi, kutoa mazingira salama na tulivu kwa mechi zote, na kukuza fursa za kielimu kupitia soka kwa wavulana na wasichana katika eneo hilo.

Mbinu hii iliyopangwa kwa umakini inalenga kujenga maendeleo endelevu ya soka huku ikitumia nguvu ya mchezo huo kuleta umoja katika mataifa yenye utofauti mkubwa wa kitamaduni ya Kusini-Mashariki mwa Asia.