Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Infantino aihakikishia timu ya taifa ya Iran kuingia Marekani

IRAN Pict

Muktasari:

  • Iran tayari imefuzu mashindano ya Kombe la Dunia 2026 kwa mara ya saba mfululizo na itashiriki fainali hizo zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico kuanzia Juni 11, 2026.

Wachezaji wa zamani wa Reading FC na Hull City, Saeed Ezatolahi na Allahyar Sayyadmanesh, wataweza kuichezea Iran katika fainali za Kombe la Dunia la 2026, endapo wataitwa kwenye kikosi cha nchi hiyo, licha ya marufuku ya raia wa taifa hilo la mashariki ya kati kuingia Marekani iliyowekwa na Rais Donald Trump.

Iran tayari imefuzu mashindano ya Kombe la Dunia 2026 kwa mara ya saba mfululizo na itashiriki fainali hizo zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico kuanzia Juni 11, 2025.

IRA 03

Habari hii ni faraja kubwa kwa kiungo wa zamani wa Reading, Ezatolahi, na mshambuliaji wa zamani wa Hull City, Sayyadmanesh, ambao sasa wana nafasi ya kuonyesha uwezo wao katika michuano hiyo mikubwa kimataifa.

IRA 01

SABABU KWA NINI DONALD TRUMP HAIWEZI KUIBANIA IRAN KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2026
Licha ya serikali ya Trump kuweka vikwazo vya usafiri vinavyohusu nchi 12 ikiwemo Iran, amri ya kiutendaji (executive order) hiyo inaitoa rasmi misafara ya michezo kama vile timu na wachezaji watakaoshiriki fainali za Kombe la Dunia 2026.

Kwa mujibu wa taarifa za ESPN, Rais Trump hana mamlaka ya kuzuia wachezaji wa timu ya taifa ya Iran, na viza zao zitatolewa ili waweze kushiriki kwenye fainali hizo.

Marufuku hiyo ya usafiri, ambayo ilianza kutekelezwa Juni 2026, inakataza kabisa raia kutoka nchi za Afghanistan, Myanmar, Chad, Jamhuri ya Kongo, Guinea ya Ikweta, Eritrea, Haiti, Iran, Libya, Somalia, Sudan, na Yemen kuingia Marekani.

IRA 02
Saeed Ezatolahi

Hata hivyo, Rais wa FIFA, Gianni Infantino, ametoa uhakika kwamba hakuna timu itakayokumbwa na matatizo ya viza kuingia Marekani kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2026.

Baada ya kutembelea chumba cha kubadilishia nguo cha timu ya Iran kufuatia mechi yao ya fainali ya CAFA Nations Cup dhidi ya Uzbekistan, Infantino amethibitisha kwamba FIFA itashughulikia masuala yote ya viza na kuhakikisha timu zote zinashiriki kikamilifu katika Kombe la Dunia.