Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fainali Kombe la Dunia kunogeshwa na hawa

DUNIA Pict

Muktasari:

  • Fainali ya Kombe la Dunia 2026, ambayo itaandaliwa kwa pamoja na Marekani, Mexico na Canada, itachezwa katika dimba la MetLife Stadium lililopo New Jersey Julai 19.

NEW JERSEY, MAREKANI: ORODHA ya mastaa watakaotumbuiza katika mechi ya fainali ya  Kombe la Dunia 2026 imetajwa rasmi, huku ikijumuisha baadhi ya wasanii wakubwa duniani pamoja na waigizaji maarufu wa kipindi cha watoto cha Muppets.

Fainali ya Kombe la Dunia 2026, ambayo itaandaliwa kwa pamoja na Marekani, Mexico na Canada, itachezwa katika dimba la MetLife Stadium lililopo New Jersey Julai 19.

Kwa kufuata utamaduni wa michezo mikubwa Marekani kama Super Bowl, mechi hiyo itakuwa na burudani maalumu ya mapumziko yenye mastaa wakubwa wa muziki duniani.

DUNI 01

Bendi ya Coldplay ilitangazwa mapema mwaka jana kuwa waimbaji wakuu wa tamasha hilo, lakini ilielezwa kuwa wangewashirikisha wasanii wengine mbalimbali katika shoo yao.

Sasa orodha kamili imetajwa kupitia video iliyomshirikisha mwimbaji wa Coldplay, Chris Martin, pamoja na mhusika maarufu wa Sesame Street, Elmo, iliyochapishwa kwenye akaunti rasmi ya kipindi hicho katika mtandao wa X.

Katika video hiyo ya kushangaza, Elmo na Cookie Monster walitangaza kuwa wataungana na Coldplay jukwaani sambamba na mastaa wengine wengi wa muziki.

DUNI 02

Miongoni mwao ni Shakira, ambaye aliimba wimbo wa Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini, Waka Waka (This Time for Africa).

Mwimbaji huyo wa Colombia pia anatarajiwa kutoa wimbo mpya wa mashindano ya mwaka huu uitwao “Dai Dai”.

Lejendi wa muziki wa pop nchini Marekani, Madonna, pia atakuwa sehemu ya tamasha hilo, akiendelea kuwa mmoja wa mastaa wakubwa duniani ikiwa ni miaka 43 sasa tangu atoe albamu yake ya kwanza.

DUNI 03

Kundi maarufu la muziki wa K-Pop kutoka Korea Kusini, BTS, pia limethibitisha kushiriki baada ya kuonekana kwenye video hiyo.

Kundi hilo lenye wanachama saba lina zaidi ya wafuasi milioni 80 kwenye Instagram na linatarajiwa kuvutia mashabiki wengi kutoka duniani kote.

Pia wasanii wa maigizo Kermit the Frog na Miss Piggy wataonekana katika tamasha hilo.