Fahamu mastaa waliobadilisha mataifa yao

LONDON, ENGLAND. TAARIFA zinaeleza kwamba mastaa wa soka ambao ni wazaliwa waa England wanaangalia uwezekano wa kubadilisha mataifa kwenda upande mwingine utakaowapa nafasi ya kucheza katika mashindano makubwa ya soka duniani kama michuano ya Euro, Afcon au Kombe la Dunia.
Nyota wa Newcastle United, Harvey Barnes huenda akakipiga katika timu ya taifa Scotland, huku mchezaji mwenzake Elliott Anderson akimfuata kwenda kucheza katika nchi hiyo.
Naye kinda anayekipiga Brighton, Evan Ferguson ameonyesha nia ya kuichezea Jamhuri ya Ireland badala ya England maarufu kama The Three Lions. Hilo siyo jambo la kushangaza kwani kuna mastaa wengine ambao walilazimika kuachana na Three Lions kwa maslahi binafsi ili tu waweze kutimiza ndoto za kwenda kucheza katika mataifa ambayo yatawapa nafasi ya kujiuza soka katika soka. Cheki hawa.
Declan Rice (Ireland/England)
Mojawapo wa mifano maarufu ni nyota wa Arsenal, Declan Rice aliiwakilisha Jamhuri ya Ireland tangu alipokuwa na umri wa miaka 16 na kupandishwa kikosi cha wakubwa. Nyota huyo alichezea taifa hilo kutokana familia yake (baba na babu) kuwa na asili ya huko. Rice aliicheza Ireland mechi tatu, lakini 2019 alitangaza kuhamia England na kuzua utata mwingi. Tangu mwaka huo amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha kocha wa England, Gareth Southgate. Kiungo huyo amecheza mechi 44 England na kufunga mabao matatu.
Jack Grealish (Ireland / England)
Huyu ni mchezaji mwingine aliyeaga taifa lake la Ireland. Kiungo huyo anayekipiga Man City alifanya uamuzi huo kama Rice. Grealish alikuwa na mwenendo mzuri na alijumuisha katika kikosi cha Ireland cha vijana wa umri wa miaka 17 na 21, na kuibuka kuwa mchezaji bora wa mwaka 2015. Licha ya kupewa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Grealish aligoma kujiunga na timu ya Ireland. Miezi kadhaa akatangaza kuwa ataicheza Three Lions. Tangu akipige katika timu hiyo ame-cheza mechi 33 na kufunga mabao mawili.
Wilfried Zaha (England/Ivory Coast)
Nyota wa zamani wa Crystal Palace, Wilfred Zaha ni mchezaji mwingie aliyepewa nafasi katika kikosi cha England. Alipewa nafasi ya kucheza dhidi ya Sweden huku England ikipokea kichapo cha mabao 4-2 mwaka 2012.
Katika mechi hiyo Zlatan Ibrahimovic alifunga bao kali la tikitaka na kuwa gumzo. Pia, Zaha alionekana kwenye mechi dhidi ya Scotland akitokea benchi miezi michache baadaye.
Kutokana na kupishana kauli kwa kocha Southgate na wakala wa winga huyo akatangaza rasmi ataichezea timu ya taifa ya Ivory Coast 2016.
Tangu wakati huo Zaha ame-ichezea Ivory Coastmechi 33 na kuifungia mabao matano katikia mashi-ndano mbambali.
Demarai Gray (England/Jamaica)
Gray alianza kuichezea timu ya vijana ya England wenye umri wa miaka 18 kabla ya kwenda kucheza mechi 26 katika kikosi cha vijana cha umri wa miaka 21. Nyota huyo aliitwa katika kikosi cha wakubwa kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Uswisi 2018. Ghafla mchezaji huyo wa zamani wa Everton na Leicester City akatengeneza pasipoti ya Jamaica kwa ajili ya kuiwakilisha na sasa amecheza mechi sita na kufunga mabao matatu.
Tariq Lamptey (England / Ghana)
Huyu ni zao lingine la vijana wa timu ya taifa la England. Mwaka 2020 nyota huyo wa zamani wa Chelsea aliwasiliana na Chama cha Soka cha Ghana ili abadili taifa la kuchezea. Lamptey aliiwakilisha Three Lions ya vijana chini ya umri wa miaka 21 kabla kupata ambayo yalikatisha maendeleo yake. Kutokana na ushindani mkubwa kwenye nafasi ya beki wa kulia na kushoto aliendelea kuiwakilisha Ghana. Pia alijumuishwa katika kikosi kilichoshiriki fainali Kombe la Dunia Qatar 2022.