Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

EUROPA LEAGUE: Fainali ya kujuana!

KUJUANA Pict
KUJUANA Pict

Muktasari:

  • Mabao mawili ya Mason Mount pamoja na mengine yaliyofungwa uwanjani Old Trafford na wakali Casemiro na Rasmus Hojlund yaliisaidia Manchester United kupata ushindi wa jumla wa mabao 7-1 dhidi ya Athletic Bilbao kwenye mechi ya nusu fainali.

LONDON, ENGLAND: MAKOCHA wawili ambao kila mmoja anapambana na hali yake, Ruben Amorim na Ange Postecoglou wataonyeshana ubabe jino kwa jino katika fainali ya Europa League ambayo itakutanisha timu mbili za England baada ya miaka sita kupita.

Mabao mawili ya Mason Mount pamoja na mengine yaliyofungwa uwanjani Old Trafford na wakali Casemiro na Rasmus Hojlund yaliisaidia Manchester United kupata ushindi wa jumla wa mabao 7-1 dhidi ya Athletic Bilbao kwenye mechi ya nusu fainali.

Wakati huo, Dominic Solanke na Pedro Porro waliihakikishia Tottenham kushinda 2-0 dhidi ya Bodo/Glimt na hivyo kutinga fainali kwa jumla ya mabao 5-1 na kwenda kuifanya Europa League ya msimu huu kuwa na fainali ya Waingereza watupu.

Kocha wa Man United, Amorim na wa Spurs, Postecoglou sasa watakutana kwenye mchezo wa fainali utakaofanyika huko Bilbao, Mei 28. Kwa kocha wa Spurs hiyo inaweza kuwa mechi ya mwisho kwenye kikosi cha Spurs baada ya kuwapo kwa imani kubwa huenda akafunguliwa mlango wa kutokea mwisho wa msimu huu hata kama timu yake itashinda na kubeba taji hilo.

Mount akiwa mwenye furaha alisema: "Haya ni mabao yangu ya kwanza Old Trafford, hivyo umekuwa usiku spesho. Ni kitu nilichokisubiri kwa muda mrefu sana. Nimekuwa na nyakati ngumu tangu nilipofika hapa kutokana na kuwa majeruhi. Lakini, nilikuwa na imani kuna kitu kizuri kitatokea na kimejitokeza kwenye nusu fainali."

Mount, bao lake la pili lilikuwa la mbali kama alilowahi kufunga David Beckham na alisema: "Nilimwona kipa ametoka golini, nilijisemea kichwani, 'unagusa moja, unapiga'. Mashabiki walikuwa wa aina yake, sasa tunarudi tena Bilbao tukitaka kumaliza kwa nguvu."

Man United na Spurs zote zimekuwa na msimu wa hovyo kwenye Ligi Kuu England, hivyo timu itakayobeba taji la Europa League itanyakua tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu pamoja na mkwanja wa Pauni 100 milioni.

Kwa pamoja timu hizo zimepoteza mechi 35 za ligi msimu huu, lakini zimekuwa na kiwango tofauti kabisa kwenye michuano ya Ulaya.

Na kocha Amorim: "Nishaanza kupata stresi tayari kwa mchezo wa fainali. Kama hatutashinda, itakuwa haina maana."

Hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa Spurs kushinda taji la Ulaya endapo itashinda tangu ilipochapwa 2-0 kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2019 dhidi ya Liverpool, mwaka ambao Chelsea pia iliichapa Arsenal 4-1 kwenye fainali ya Europa League.

Solanke alisema: "Najisikia vizuri sana. Tumemaliza kazi na sasa tupo fainali. Bado mechi moja tu!"

Spurs inaamini itafanya vizuri kwenye mchezo huo wa fainali baada ya kushinda mechi zote tatu ilizokutana na Man United msimu huu.

MECHI ZA SPURS,

MAN U MSIMU HUU

Man U 0-3 Spurs - Sept 29, 2024

Spurs 4-3 Man U - Dec 19, 2024

Spurs 1-0 Man U - Feb 16, 2025