Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Eti Nagelsmann apewe Man City

NINGE Pict

Muktasari:

  • Kiungo wa zamani wa Man City na Ujerumani, Didi Hamann ameitaka klabu yake hiyo kumchukua Mjerumani mwenzake endapo kama itaamua kuachana na Pep Guardiola.

MANCHESTER, ENGLAND: MABOSI wa Manchester City wameambiwa wamchukue Julian Nagelsmann akarithi mikoba ya Pep Guardiola - uamuzi ambao unaweza kumpa fursa Jurgen Klopp kwenda kunasa ajira ya kuinoa Ujerumani.

Kiungo wa zamani wa Man City na Ujerumani, Didi Hamann ameitaka klabu yake hiyo kumchukua Mjerumani mwenzake endapo kama itaamua kuachana na Pep Guardiola.

Hata hivyo, anaamini Nagelsmann hawezi kukubali kibarua cha kwenda kuinoa Man City kwa sasa hadi fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakapomalizika.

Klopp, ambaye aliachana na Liverpool mwishoni mwa msimu wa 2023-24, alisema hana mpango wa kurudi tena kufanya kazi kwenye Ligi Kuu England. Soka la kimataifa ni kitu kingine anachoweza kukifikiria Klopp, hasa kama timu yenyewe itakuwa Die Mannschaft.

Klopp, 57, kwa sasa anafanya kazi Red Bull, ambako amekuwa mkuu wa soka wa klabu za kampuni hiyo tangu Januari. Kumekuwa na kama kama nyingi kwenye ishu ya Guardiola juu ya maisha na hatima yake Man City msimu huu, lakini Hamann anaamini Nagelsmann anafaa kwenda kupewa kazi na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England.

"Nagelsmann anaweza kuwa chaguo sahihi kwa sababu naamini hapa Pep atakuwa na maoni chanya juu ya Nagelsmann," alisema Hamann.

Kinachoaminika ni kwamba Guardiola atatoa mapendekezo ya kocha atakayetaka kuja kuchukua mikoba yake wakati atakapoamua kuachana na miamba hiyo ya Etihad.