Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Eti Amorim tayari, bado familia ya Glazer

BOSI Pict

Muktasari:

  • Pia amependekeza kuwa familia ya Glazer huenda ikawa inayofuata kuondoka kwenye klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford.

MANCHESTER, ENGLAND: BOSI wa mchezo wa masumbwi wa Saudi Arabia, Turki Alashikh, anaonekana kufurahia kuondoka kwa Ruben Amorim katika klabu ya Manchester United.

Pia amependekeza kuwa familia ya Glazer huenda ikawa inayofuata kuondoka kwenye klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford.

Manchester United walimfuta kazi Amorim, Jumatatu asubuhi kufuatia kauli yake kali na ya kushangaza baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Leeds United.

Mheshimiwa Alashikh hakupoteza muda kutoa maoni yake, akielekea moja kwa moja kwenye mtandao wa X (zamani Twitter).

Amesema: “Alhamdulillah… hatimaye… na familia ya Glazer nao wafuatie hivi karibuni.”

Alashikh ameendelea kuonyesha nia kuhusu umiliki wa Man United, ingawa haijabainika iwapo anawapenda au hapendi wamiliki wa sasa. Oktoba mwaka jana, Alashikh aliandika kwenye X kuhusu umiliki wa Man United: “Habari bora niliyosikia leo ni kwamba Man United wako katika hatua za mwisho za kukamilisha makubaliano ya kuuzwa kwa mwekezaji mpya. Natumaini atakuwa bora kuliko wamiliki wa awali.”

Familia ya Glazer bado haipendwi na mashabiki hadi leo, lakini Jim Ratcliffe na kampuni ya INEOS pia hawajafanikiwa kuwavutia wengi.

Man United walitengana na Amorim baada ya uhusiano wake na mkurugenzi wa soka, Jason Wilcox kuvunjika. Amorim alitoa maneno makali wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Leeds.

Amesema: “Nilikuja hapa kuwa meneja wa Man United, siyo kocha wa Man United. Na hilo liko wazi.

“Ninajua jina langu si Tuchel, si Conte, wala si Mourinho, lakini mimi ni meneja wa Man United. Na itakuwa hivyo kwa miezi 18, au mpaka bodi iamue kubadilisha.”

Hata hivyo, bodi ya Man United iliamua kubadilisha mambo baada ya saa 24 tu, siyo miezi 18.