Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Erling Haaland azua 'balaa' Peru

HALAAND Pict

Muktasari:

  • Haaland alikuwa mmoja wa nyota waliovutia zaidi kwenye Kombe la Dunia 2026, akifunga mabao saba kabla ya safari ya Norway kusimamishwa na England katika hatua ya robo fainali.

DALLAS, MAREKANI: MSHAMBULIAJI wa Norway, Erling Haaland, ameibuka kuwa gumzo nchini Peru baada ya mamia ya wazazi kuwapa watoto wao majina yanayotokana na nyota huyo wa Manchester City.

Haaland alikuwa mmoja wa nyota waliovutia zaidi kwenye Kombe la Dunia 2026, akifunga mabao saba kabla ya safari ya Norway kusimamishwa na England katika hatua ya robo fainali.

Licha ya Norway kutolewa, kiwango chake kimeonekana kuwavutia wengi nchini Peru, taifa ambalo hata halikufuzu kushiriki Kombe la Dunia.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Taifa ya Usajili wa Vitambulisho na Hali za Kiraia ya Peru (Reniec), zaidi ya watoto 500 nchini humo wamepewa majina yanayohusiana na Haaland.

HAAL 01

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa watoto 468 wamepewa jina Haaland, huku wengine 91 wakipewa jina lake kamili la Erling Haaland.

Idadi hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita, huku ikitarajiwa kuongezeka kutokana na umaarufu unaoendelea wa mshambuliaji huyo.

HAAL 02

Mabao dhidi ya Brazil yachochea umaarufu

Umaarufu wa jina la Haaland uliongezeka zaidi baada ya nyota huyo kuifungia Norway mabao mawili dhidi ya Brazil, ushindi uliowatoa mabingwa hao wa dunia kwenye mashindano.

Msemaji wa Reniec, Ivan Torres, alisema si jambo la ajabu kwa wazazi nchini Peru kuwapa watoto wao majina ya mastaa wa soka wanaowavutia.

"Wachezaji mbalimbali wa soka wamekuwa chanzo cha msukumo kwa Waperu kuwapa watoto wao majina yao," alisema Torres.

HAAL 03

Messi, Ronaldo na Neymar nao wanatikisa

Haaland amejiunga kwenye orodha ya mastaa wa soka ambao majina yao yamekuwa maarufu nchini Peru.


Kwa mujibu wa Reniec: Messi ana watoto 3,402 wenye jina hilo.

Ronaldo (kwa heshima ya Cristiano Ronaldo) ana watoto 1,185.

Kinara wa orodha hiyo ni Neymar, ambaye jina lake linabebwa na karibu watoto 34,000 nchini Peru.

Ingawa Peru haikuwapo kwenye Kombe la Dunia 2026, inaonekana mashabiki wake wameendelea kuishi na burudani ya soka kwa njia ya kipekee, kwa kuwapa watoto wao majina ya nyota wanaowavutia zaidi duniani.