Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haaland: Presha ipo kwa England

HAALAND Pict

Muktasari:

  • Norway imeandika historia kwa kufika robo fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu iliposhiriki fainali za mwaka 1998. Baada ya kumaliza nafasi ya pili Kundi I, iliwatoa Ivory Coast na Brazil katika hatua za mtoano.

MIAMI, MAREKANI: NAHODHA na mshambuliaji ya Norway, Erling Haaland, amesema presha yote ipo kwa England kuelekea mchezo wa robo fainali ya Kombe la Dunia utakaochezwa Jumamosi, huku akiwasihi waandishi wa habari kuongeza shinikizo zaidi kwa kikosi cha Thomas Tuchel.

Norway imeandika historia kwa kufika robo fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu iliposhiriki fainali za mwaka 1998. Baada ya kumaliza nafasi ya pili Kundi I, iliwatoa Ivory Coast na Brazil katika hatua za mtoano.

Kwa upande wa England, imekuwa ikipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa baada ya kufika angalau robo fainali katika Kombe la Dunia tatu zilizopita, ingawa haijatinga fainali tangu ilipotwaa ubingwa mwaka 1966.

HAA 01

Alipoulizwa kama presha yote ipo kwa England, Haaland hakusita kujibu:

“Ndiyo, bila shaka. Nafikiri kuna timu chache zinazotajwa kuwa mabingwa watarajiwa, na England ni mojawapo.”

Kisha akawageukia waandishi wa habari kwa utani na kusema:

“Nadhani nyinyi wote mnapaswa kuwawekea presha kubwa kabisa wachezaji wa England.”

HAA 02

Aliendelea:”Mashabiki wao wanapaswa kuwa na imani kwamba watafuzu. Ni England.”

Haaland kwenye moto wa mabao

Mshambuliaji huyo wa Manchester City mwenye umri wa miaka 25 amefunga katika kila moja ya mechi zake 14 zilizopita za mashindano akiwa na Norway.

Sasa atakuwa na kazi ya kuendeleza rekodi hiyo dhidi ya nchi alikozaliwa, England. Haaland alizaliwa mjini Leeds wakati baba yake, Alf-Inge Haaland, alipokuwa akihama kutoka Leeds United kwenda Manchester City.

Timu hizo zitakutana Jumamosi mjini Miami.

“Hata mimi sikutarajia kufika hapa”

Mwaka jana, Haaland aliliambia jarida la Time kwamba aliipa Norway nafasi ya asilimia 0.5 pekee ya kutwaa Kombe la Dunia.

Lakini sasa mambo yamebadilika. Mabao saba aliyofunga katika mechi nne, yakiwemo mawili dhidi ya Brazil hatua ya 16 Bora, yameivusha Norway hadi robo fainali.

HAA 03

“Kwa kweli sikutarajia hili. Kufika robo fainali ya Kombe la Dunia na Norway ni jambo la kushangaza hata kwangu.”

Aliongeza:”Kucheza dhidi ya Brazil ilikuwa ndoto kwa Wanorway wengi, halafu tukawafunga na sasa tunaenda kucheza na England kwenye robo fainali nchini Marekani. Hili ni jambo la kipekee sana.”

“Ni vigumu kuelewa ukubwa wa tukio hili, kwa sababu lazima uingie uwanjani na kucheza kama ni mazoezi ya kawaida.”

“Ukiona namna watu walivyosherehekea Norway, utaelewa kwamba hali kama hii si ya kawaida kwetu. Ni tukio la kipekee sana.”

Marekani imemvutia Haaland

Umaarufu wa Haaland nchini Marekani umeongezeka maradufu wakati wa mashindano haya, si kwa mabao yake pekee bali pia kwa maisha yake nje ya uwanja. Saa chache baada ya kuifungia Norway ushindi dhidi ya Ivory Coast, alionekana akifanya manunuzi ya kofia na buti za Cowboy mjini Dallas.

Video ya ziara hiyo aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa YouTube ilifikisha zaidi ya watazamaji milioni sita ndani ya siku tano.

Akizungumzia mapokezi aliyoyapata Marekani amesema:

“Ninawapenda Wamarekani. Wana ucheshi wa kipekee na huwa wananifurahisha, ndiyo maana napenda tabia yao.”

Aliendelea:”Kwa ujumla kila kitu kuhusu Kombe hili la Dunia hapa Marekani kimekuwa cha kuvutia. Mechi, viwanja, mazingira ya mazoezi, kila kitu kimekuwa bora sana. Nimefurahia sana na nimevutiwa.”

Mbali na hilo, Haaland pia alionekana akihudhuria fainali ya Stanley Cup huko North Carolina pamoja na kuwaongoza wenzake kufanya shangwe maarufu ya Viking Row baada ya ushindi dhidi ya Brazil.

“Maisha si soka pekee”

Haaland amesema moja ya siri ya mafanikio yake ni kupenda kufurahia maisha hata katikati ya mashindano makubwa.

“Napenda kufanya utani na kufurahia maisha. Hilo ni jambo muhimu kwangu kila siku.”

“Ni kweli lazima ufanye mazoezi vizuri, uwe makini na ujitayarishe vizuri, lakini pia unapaswa kufurahia kila wakati unaoupata.”

Alimalizia kwa kusema:

“Hivyo ndivyo tumekuwa tukifanya hapa. Tunacheza Kombe la Dunia, pia tunafurahia kila dakika kwa sababu hakuna jambo linalodumu milele. Lazima tufurahie nafasi hii wakati bado ipo.”