Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

EPL yashtua kufuta ujumbe unaomhusu Slot

EPL Pict

Muktasari:

  • Kocha Slot na msaidizi wake Spike Hulshoff walimvamia mwamuzi Michael Oliver baada ya filimbi ya mwisho kwenda kupinga bao la James Tarkowski alilofunga kwenye dakika za majeruhi kwenye mechi yao ya Merseyside derby uwanjani Goodison Park wiki iliyopita.

LONDON, ENGLAND: LIGI Kuu England imeibua mkanganyiko baada ya kufuta baadhi ya maneno yaliyopo kwenye taarifa yao rasmi iliyopo kwenye mtandao wao inayobainisha Kocha wa Liverpool, Arne Slot atakabiliwa na adhabu ya kufungiwa mechi mbili.

Kocha Slot na msaidizi wake Spike Hulshoff walimvamia mwamuzi Michael Oliver baada ya filimbi ya mwisho kwenda kupinga bao la James Tarkowski alilofunga kwenye dakika za majeruhi kwenye mechi yao ya Merseyside derby uwanjani Goodison Park wiki iliyopita.

Liverpool ilidai kulikuwa na faulo wakati bao hilo linatengenezwa, lakini mwamuzi Oliver alilikubali, uamuzi ulioungwa mkono na VAR katika mechi iliyomalizika kwa Liverpool kufungana na Everton mabao 2-2.

Ligi Kuu England ilifichua juzi Alhamisi asubuhi Slot alionyeshwa kadi nyekundu katika mechi hiyo kutokana na kutumia lugha chafu dhidi ya mwamuzi na taarifa hiyo ilibainisha:

"Kocha mkuu wa Liverpool, Arne Slot alionyeshwa kadi nyekundu mwishoni mwa mchezo wa Merseyside derby kutokana na kutumia lugha chagu. Amefungiwa mechi mbili."

Adhabu hiyo inaweza kubaki kama ilivyo, lakini kilichochangaza watu ni kitendo cha Ligi Kuu England kufuta taarifa hiyo kwenye tovuti yao. Kuna taarifa zinadai taarifa ya adhabu ilitoka haraka, hivyo pengine inasubiriwa ripoti ya waamuzi kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho, kwamba adhabu inaweza kuwa kubwa zaidi ya ile ya mechi mbili kutokana na kuonyeshwa kadi nyekundu.

Baada ya kadi hiyo nyekundu, Slot hakuzungumza na waandishi wa habari baada ya mechi hiyo ya Jumatano kulingana na kanuni za Ligi Kuu England. Kocha wa kikosi cha kwanza, Jonny Heitinga sasa atawajibika kwa ajili ya mechi ya kesho Jumapili dhidi ya Wolves.

Na huenda akabaki kwenye benchi la ufundi kwa mechi ya Jumatano ijayo dhidi ya Aston Villa, kama Slot na Hulshoff wataendelea kutumikia adhabu yao ya kufungiwa mechi mbili. Lakini, kuna uwezekano pia Slot akaendelea kukaa kwenye benchi katika mechi ya Wolves.

Liverpool inaweza kutozwa faini pia kutokana na wachezaji wake kuonyeshwa kadi sita za njano katika mechi moja, huku ikiwamo kadi nyekundu kwa makocha na mchezaji Jones. Faini ya makosa kama hayo ni Pauni 25,000.