Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

EPL inaendelea tena, ngojeni muone

EPL Pict
EPL Pict

Muktasari:

  • Kuna mengi yanatarajiwa kutokea katika wiki hii na hapa tumekuletea mambo matano muhimu kuelekea wikiendi hii  ikiwa pamoja na rekodi, ratiba kamili na kile kinachoweza kutokea.

LONDON, ENGLAND: BAADA ya utamu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League katikati ya wiki hii, utamu wa Ligi Kuu England umerejea tena leo ambapo timu zote zitashuka dimbani baada ya jana Brighton kufungua dimba dhidi ya Southampton.

Kuna mengi yanatarajiwa kutokea katika wiki hii na hapa tumekuletea mambo matano muhimu kuelekea wikiendi hii  ikiwa pamoja na rekodi, ratiba kamili na kile kinachoweza kutokea.


NI AMORIM TENA

Baada ya kupata ushindi wake wa kwanza akiwa kocha wa Manchester United kwa kuifunga 3-2 Bodo/Glimt katika mechi ya Europa League juzi, Ruben Amorim anarudi tena kwenye EPL wikiendi hii dhidi ya Everton kujaribu kuwaaminisha mashabiki wa Mashetani Wekundu kwamba yeye ni mtu sahihi wa kuirejesha klabu hiyo katika zama bora.

Rasmus Hojlund aliweka chuma mbili baada ya Alejandro Garnacho kuitanguliza United mapema tu katika dakika ya kwanza kwenye Uwanja wa Old Trafford na kuiwezesha timu yao kushika nafasi ya 12 katika msimamo wa Europa League ikiwa ikiwa na pointi tisa. Vinara ni Lazio wenye pointi 13 baada ya kila timu kucheza mechi tano.

Alipata sare isiyotarajiwa katika mechi yake ya kwanza ya ligi dhidi ya Ipswich, na sasa kesho Amorim atakutana na kipimo kingine cha ugumu wa EPL dhidi ya Everton.

Licha ya kufanya vibaya katika kipindi chake, mtangulizi wake Erik ten Hag hakuwahi kupoteza mechi yoyote ya kimashindano mbele ya Everton ambayo haijapata ushindi dhidi ya Man United tangu Aprili 2022.

Everton pia haijawahi kushinda mechi yoyote ya Ligi Kuu England dhidi ya Man United katika dimba la Old Trafford, hivyo Amorim akipoteza atakuwa ameanza na rekodi moja mbaya kabisa.

Kwa sasa Everton ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 11, wakati Man United iko nafasi ya 12 kwa pointi 16.

Man United ikishinda inaweza kupanda hadi nafasi ya sita, lakini Everton haitosogea popote hata ikipata pointi tatu ingawa ikipoteza inaweza kushushwa hadi nafasi tatu za mwisho.

Mchezo huu unatarajiwa kupigwa kesho, saa 10:30 jioni huku takwimu zikionyesha katika mechi tano za mwisho dhidi ya Everton, Man United imeshinda zote.


GUARDIOLA ATAJITETEA?

Hali imezidi kuwa mbaya kwa Pep Guardiola. Mara yamwisho kuonja ladha ya ushindi ilikuwa mwezi uliopita iliposhinda dhidi ya Southampton kwa bai 1-0, baada ya hapo imecheza mechi sita, ikifungwa tano mfululizo na kutoa sare moja.

Mtihani mgumu mbele ni dhidi ya majogoo wa Jiji la Liverpool ambao ndio wapo pamoja nao katika mbio za kuliwania taji la Ligi Kuu England msimu huu.

Man City inashika nafasi yapili ikiwa na pointi 23 wakati Liverpool ikiongoza kwa pointi 31. Ikiwa mechi hii itamalizika kwa Man City kufungwa, Liverpool itakuwa imejichimbia kileleni kwa tofauti ya pointi 11.

Baada ya kupoteza mchezo uliopita wa Ligi Kuu, Guardiola alisema ikiwa watapoteza mchezo huu basi rasmi watakuwa wameaga safari ya kuliwania taji la EPL msimu huu.

Msimu huu Man City inatafuta taji lao la tano mfululizo  la EPL ingwa hadi sasa mambo yanaonekana kuwa magumu.

Jambo bata kwa Man City ni kwamba wanaenda kukutana na Liverpool ambayo imekuwa katika kiwango bora tangu kuanza kwa msimu.

Katika mechi 14 zilizopita imeshinda 13 na kutoa sare moja mara ya mwisho kupoteza mchezo wa kimashindano ilikuwa ni Septemba 14 ilipokutana na Nottingham Forest.

Ikiwa itafungwa mechi hii itakayopigwa katika dimba la Anfield itakuwa ni mara ya kwanza kwao kupoteza mbele ya Man City kwenye uwanja huo tangu mwaka 2019.


LOPETEGUI NI MAAJABU TENA

Wiki iliyopita kocha wa West Ham alibadilisha upepo baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle United.

Kabla ya mechi hii alionekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kufungashiwa virago ikiwa angepoteza lakini aliondoa hali hiyo kwa ushindi.

Wiki hii ni kipimo chake kingine na mbaya zaidi atakuwa anakutana na Arsenal ambayo imeonekan kurudi kaitka mstari baada ya kufanya vibaya wiki kadhaa zilizopita.

Katika mchezo huu ambao utapigwa katika dimba la London Studium, West Ham ambayo ipo nafasi ya 14 ikiwa na alama 15, ikiwa itapanda hadi nafasi ya tisa ingawa itategemea na matokeo ya timu nyingine zilizopo juu yao kuanzia nafasi hiyo hadi namba tisa.

Kwa upande wa Arsenal kama itashinda mechi hii inaweza kuishusha Man City ambayo itakuwa na kibarua kigumu mbele ya Liverpool. Mechi itaanza kupigwa saa 2:30 usiku.


IPSWICH ITAENDELEA

Kabla ya mechi za wiki iliyopita mmoja kati ya makocha waliokuwa wanatajwa kwamba wamekalia kuti kavu ni  Kieran McKenna wa Ipswich kutokana na matokeo ya timu yake iliyopo nafasi ya 18 kwenye mstari mwekundu wa kushuka daraja.

Hata hivyo, walishangaza watu wengi baada ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Manchester United iliyokuwa chini ya kocha mpya.

Raundi hii inakutana na Nottingham Forest. Hii itakuwa ni mechi nyingine ya kipimo kwa  Kieran McKenna ambaye anahitaji kujiondoa katika eneo la hatari kwenda juu zaidi.

Ingawa inaonekana kuwa na ugumu kwani itakutana na Nottingham ambayo tangu kuanza kwa msimu huu imekuwa moja kati ya timu bora ndani ya EPL ingawa hivi karibuni inapitia wakati mgumu baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo za ligi.

Ushindi kaitka mchezo huu unaweza kuwapandisha Ipswich hadi nafasi ya 15 ambayo kwa sasa inakaliwa na Everton yenye pointi 11.

Pia itategemea na matokeo ya timu nyingine zilizopo nafasi ya 17 na 16 ambazo ni Wolves na Newcastle United.


MSIMAMO MAJANGA

Utamu zaidi unaofanya watu wasipange kukosa kuangalia mechi za wikiendi hii ni msimamo ulivyo. 

Kuanzia timu inayoshika nafasi ya 19 hadi nafasi yapili yoyote inaweza ikashushwa kutoka nafasi iliyopo kwenda chini ikiwa itapoteza mchezo.

Timu ya 19 ambayo ni Crystal palace yenye pointi nane, ikiwa itashinda dhidi ya Newcastle Jumapili inaweza kupanda hadi nafasi ya 17 au 16 mahali ambako ni salama.

Vilevile timu za katikati ya msimamo ambazo ni kuanzia nafasi ya 14 hadi ya sita, yoyote ile itakayopoteza inaweza kujikuta ikiondoshwa kabisa kwenye 10 bora na hata kuangukia ilipo West Ham.

Kwa mfano, Man United iliyipi nafasi ya inaweza kupanda hadi nafasi ya sita kwa Tottenham ikiwa itapoteza mchezo wake.

Kwa upande wa timu za juu kuanzia kwa Brighton inayoshikilia nafasi ya tano hadi kwa Man City inayoshika nafasi yapili yoyote inaweza inaweza kupanda na kushuka kwani tofauti ya Brighton na Man City ni pointi moja tu, hivyo itakayotoa sare ama kufungwa inaweza kujikuta kwa Brighton ama itapanda hadi ilipo Man City.


RATIBA KAMILI

LEOO, JUMAMOSI

Brentford            vLeicester City    (Saa 12:00 Jioni)

C.Palace               vNewcastle (Saa 12:00 Jioni)

Forest                  vIpswich              (Saa 12:00 Jioni)

Wolves                vBournemouth    (Saa 12:00 Jioni)

West Ham           vArsenal              (Saa 2:30 Usiku)


KESHO, JUMAPILI

Chelsea                vAston Villa        (Saa 10:30 jioni)

Man United         vEverton             (Saa 10:30 Jioni)

Tottenham          vFulham              (Saa 10:30 Jioni)

Liverpool             vManchester City         (Saa 1:00 Usiku)