Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

EPL 2025/25 imeanza kibabe sana

EPL Pict

Muktasari:

  • Rekodi ya kwanza ni ile ya wiki ya kwanza ya ufunguzi wa EPL msimu huu, jumla ya wachezaji saba waliokuwa wanacheza ligi hii kwa mara ya kwanza walifunga. Mara ya mwisho kutokea jambo kama hili ni msimu wa 1992/93.

LONDON, ENGLAND: YES. Mzigo ulirudi rasmi wiki iliyopita. Waliolia wamelia, waliocheka wamecheka, lakini mbali ya mato-keo ambayo yalitokea kwa timu mbalimbali, pia kuna rekodi kibao zilizowekwa na timu pamona na wachezaji.

Rekodi ya kwanza ni ile ya wiki ya kwanza ya ufunguzi wa EPL msimu huu, jumla ya wachezaji saba waliokuwa wanacheza ligi hii kwa mara ya kwanza walifunga. Mara ya mwisho kutokea jambo kama hili ni msimu wa 1992/93.

Tangu kuanza kwa msimu wa 2023/24 Arsenal ndiyo timu iliyofunga mabao mengi zaidi (31) kutokana na kona wakati Manchester United ndiyo timu iliyofungwa mabao mengi ya aina hiyo (23).

Vile vile Man United imekuwa timu ya pili kufungwa na Mikel Arteta mara nyingi zaidi (8), baada ya Wolves inayoshika nafasi ya kwanza na ameifunga mara tisa akiwa kama kocha mkuu.

Katika mchezo wa Chelsea na Crystal Palace kulikuwa na mashuti 31 ambayo yalipigwa nje ya lango. Mechi hii iliweka rekodi ya kuwa mechi ya pili kuwa na mashuti mengi yaliyotoka nje ya lango lakini ikashindwa kuzalisha bao.

Mchezo wa mwisho kuwa na mashuti mengi kama hayo ilikuwa msimu wa 2018/19 na Burnley ilikutana na Southampton.

Kiungo Morgan Gibbs-White rasmi amekuwa mmoja kati ya wachezaji wawili katika historia ya Not-tingham Forest ambao wametoa asisti nyingi zaidi Ligi Kuu England. Staa huyu ametoa asisti 27 hadi sasa sawa na Ian Woans.

Josh Acheampong mwenye umri wa miaka 19 na siku 104 baada ya kuanza mchezo wa kwanza wa ligi dhidi Crystal Palace akiichezea Chelsea, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kuanza mechi ya EPL katika historia ya Chelsea baada Glen Johnson kuweka rekodi hiyo msimu wa 2003/04 akiwa na um-ri wa miaka 18 na siku 359.

Katika mwezi huu, Erling Haaland amefunga mabao 21 ya Ligi Kuu England ambayo ni mabao mengi zaidi ndani ya mechi chache.

Mch ezaji ambaye anaongoza kwa kufunga mabao mengi ya EPL mwezi huu ni Andrew Cole ambaye amefunga mabao 25 katika mechi 44, akifuatiwa na Les Ferdinand ambaye alifinga mabao 22 katika mechi 47.

Timu iliyopanda daraja, Sunderland ilimaliza katika nafasi ya pili Jumamosi ya wiki iliyopita na ilikuwa ni mara yao ya kwanza kufanya hivyo tangu mwaka 2001.