Embiid ampiga Lebron Olimpiki

Muktasari:
- Tukiwa ndani ya mbio za 12 za kuugawa msimu kabla ya kwenda mapumziko marefu, tayari mabingwa saba tofauti wamepatikana ikiwa ni wengi zaidi tangu mara ya mwisho mwaka 2012 waliposhinda madereva wanane.
KWA wanaofuatilia mbio za magari duniani (formula one) mwaka huu, basi wapo kwenye kilele cha msisimko mkubwa uliopo kwenye mbio hizo msimu huu.
Tukiwa ndani ya mbio za 12 za kuugawa msimu kabla ya kwenda mapumziko marefu, tayari mabingwa saba tofauti wamepatikana ikiwa ni wengi zaidi tangu mara ya mwisho mwaka 2012 waliposhinda madereva wanane.
Hii ni kutokana na Oscar Piastri wa McLaren kushinda mbio ya Hungary Jumapili iliyopita, ikimpa rekodi ya dereva mdogo na wa kwanza aliyezaliwa karne ya 21 kushinda mbio hizo, akiwa amezaliwa mwaka 2001.
Utamu zaidi, Piastri alifuatiwa na dereva mwenza wa McLaren, Lando Norris nafasi ya pili, wakiweka rekodi mpya ya madereva wa kampuni moja kufuatana tangu mara ya mwisho mwaka 2001 walipofanya hivyo Ralf Schumacher na Juan-Pablo Montoya wa Williams.
Lewis Hamilton wa Mercedes hatimaye alimaliza nafasi ya tatu ikiwa ni ndani ya podium, ikimpa rekodi kubwa maradufu ya kufikisha podium 200, hakuna dereva aliyewahi kufikisha idadi hiyo kwani Michael Schumacher aliishia podium 155 pekee.