Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Durant staa wa nane NBA kufikia rekodi ya 31,000

NBA Pict

Muktasari:

  • Mwamba Durant alifikia rekodi hiyo wikiendi hii wakati wa mchezo kati ya Houston Rockets na Phoenix Suns uliopigwa mjini Houston ambao ulimalizika kwa Rockects kuvuna pointi 117-98.

HOUSTON, MAREKANI: KEVIN Durant amekuwa mchezaji wa nane katika historia ya Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) kufikisha pointi 31,000, lakini simulizi tamu ni namna alivyofikia rekodi hiyo.

Mwamba Durant alifikia rekodi hiyo wikiendi hii wakati wa mchezo kati ya Houston Rockets na Phoenix Suns uliopigwa mjini Houston ambao ulimalizika kwa Rockects kuvuna pointi 117-98.

Mchezaji huyo anayeichezea Rockets aliingia kwenye mchezo huo akihitaji pointi nne kufikia rekodi hiyo, ambapo alipata alama zake za kwanza kwa mitupo miwili ya adhabu kabla ya kufanikisha hilo aliporuka na ‘jump shot’ katikati ya robo ya kwanza.

AB 04

Durant mwenye umri wa miaka 37, amefanikisha hilo katika mchezo wake wa 1,141 akiungana na mfungaji bora wa muda wote wa NBA, LeBron James kufikia alama 31,000 katika idadi ya tatu ndogo ya michezo nyuma ya Michael Jordan (1,011) na Wilt Chamberlain (1,015).

Mastaa wengine waliofikisha angalau alama 31,000 ni Kareem Abdul-Jabbar, Karl Malone, Kobe Bryant na Dirk Nowitzki na hivyo kuonyesha ni kwa namna kufikia idadi hiyo ya pointi ni kazi kubwa.

Durant ambaye alichaguliwa wa pili kwenye drafti 2007, yupo katika msimu wake wa kwanza na Rockets baada ya dili kubwa la uhamisho kutoka Phoenix majira ya kiangazi yaliyopita.

AB 03

Wakati wa mchezo huo Durant alionekana kwamba alikuwa amepania kufanya jambo, kwani mipira mingi aliyokuwa akitoa kama pasi kwa wenzake aliiomba haraka haraka na kukimbia kwa kasi kuelekea upande wa wapinzani wao.

Na kana kwamba wachezaji wenzake kikosini walikuwa upande wake kila mara walikuwa wakimtupia mpira na kupambana kuhakikisha kwamba anazifikia nyavu za Phoenix ingawa hakuwa na maajabu mengi uwanjani.

Katikati ya rekodi hiyo, Durant aliyeichezea Phoenix kwa miaka miwili (2023-2025) akitokea Brooklyn Nets iliyomsajili kutokea Golden State Warriors ameipata akiwafunga waajiri wake wa zamani katika mchezo wa kwanza tu tangu aachane nao.

AB 02

Mwamba huyo aliyechaguliwa kwenye drafti na Seattle SuperSonics ana rekodi zaidi ya 40 za kikapu ikiwamo ubingwa wa NBA mara mbili (2017 na 2018) miaka ambayo pia aliibuka kuwa MVP wa fainali zilizompa ubingwa akiwa  Golden State Warriors.


KNICKS WAPO

Wakati Durant akisherehekea mafanikio hayo, New York Knicks waliuanza mchezo kwa kuandika ya 23-0 dhidi ya Utah Jazz ikiwa ni rekodi ya kibabe zaidi tangu NBA ianze kurekodi kwa undani kila tukio.

Knicks waliifanyia Jazz kile kilichoonekana kuwa mashambulizi makali kwa kuanza mchezo kwa uongozi wa pointi 23-0  ambao ni mwanzo mzuri zaidi katika NBA tangu ligi ianze kurekodi matukio ya mchezo kwa undani katika robo zote nne.

Knicks waliizuia Jazz kutopata pointi nusu ya robo ya kwanza na walikuwa mbele kwa alama 28 robo hiyo ilipomalizika.

AB 01

Karl-Anthony Towns alianza kufunga kwa mtupo wa pointi tatu na Jalen Brunson alifunga mwingine katikati ya robo ya kwanza Knicks walikuwa wamefunga pointi 23. Hiyo ilikuwa rekodi ya alama nyingi zilizowahi kufungwa na timu moja kabla ya nyingine kupata pointi tangu 1997, NBA ilipoanza kurekodi matukio kwa undani katika mchezo.

Jazz walikosa mitupo 12 ya mwanzo kabla ya Keyonte George kuwafungulia akaunti ya pointi kwa kufunga ‘three-point play’ ikiwa imesalia dakika 5:27 kwenye robo. Ilikuwa pointi 41-13 baada ya robo ya kwanza, huku uongozi wa alama 28 pia ukiwa mkubwa zaidi kwa Knicks katika kipindi cha play-by-play. Hadi mwisho wa mchezo Knicks walikuwa na pointi 146-112.

Jazz pia waliwahi kuadhirika kwa pengo jingine la alama 28 baada ya robo ya kwanza msimu huu pale Minnesota waliongoza 43-15 katika ushindi wao wa 137-97 Novemba 7.