Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cunningham anavyousaka u-MVP NBA kimyakimya

MVP Pict

Muktasari:

  • Cunningham amefika kileleni, na huu ni mwanzo tu wa nyota huyo wa Detroit anayepaa kwa kasi katika mchezo huo, kwani Pistons inajijenga kwa sasa kumzunguka nyota huyo mwenye umri wa 24.

MOTOR CITY, MAREKANI: KADRI Detroit Pistons wanavyoendelea kufufuka kama timu makini NBA, Cade Cunningham, kwa upande mwingine amekuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi katika Ligi ya Kikapu Marekani.

Cunningham amefika kileleni, na huu ni mwanzo tu wa nyota huyo wa Detroit anayepaa kwa kasi katika mchezo huo, kwani Pistons inajijenga kwa sasa kumzunguka nyota huyo mwenye umri wa 24.

Miaka michache iliyopita Pistons ilikuwa katika kiwango duni ikimaliza nafasi mbili za mwisho, lakini imeendelea kupambana kujikwamua na kujiweka katika nafasi bora ili kurudi katika enzi zile ilipokuwa tishio kwa vigogo.

Cunningham, aliyechaguliwa kwenye drafti ya 2021, alikuwa na msimu wa kwanza uliovunja moyo huku Pistons ikimaliza na ushindi wa michezo 23 kati ya 59 na kuwa timu ya tatu ya mwisho katika ligi.

MV 01

Lakini, msimu wake wa pili ulikuwa mbaya zaidi baada ya kupata jeraha la mguu lililomaliza msimu wake, huku timu ikimaliza ikiwa na rekodi mbaya zaidi NBA  ikishinda mechi 17 na kupoteza 68.

Ungeweza kufikiria mambo yasingeweza kuwa mabaya zaidi, lakini yalizidi kuwa mabaya. Pistons ilimaliza na ushindi wa mechi 14 kati ya 68 katika msimu wa 2023–24, rekodi mbaya zaidi katika historia ya klabu, na wakaandika rekodi ya muda mrefu zaidi ya kupoteza michezo mfululizo NBA zikifikia 28.


KUIBUKA

Baada ya msimu mbaya, Pistons walifukuza watu kibao uongozini na sasa John-Blair Bickerstaff ndiye anayeiongoza timu akiwa kocha mkuu. Ujio wake ulikuwa na mafanikio ya haraka, kwani waliongeza ushindi mpaka mechi 30 kutoka msimu uliopita na kumaliza wakiwa nafasi ya sita.

Mmoja wa wachambuzi wa NBA, Marc Stein alipozungumza na talkSPORT hivi karibuni kuhusu kuibuka kwa Pistons, amesema:

“Pistons walikuwa bora zaidi NBA msimu uliopita baada ya kupitia msururu wa kupoteza mechi nyingi msimu uliotangulia, ambayo ndiyo rekodi ndefu zaidi ya kupoteza mechi mfululizo katika historia ya NBA,” amesema Stein.

MV 02

Stein pia alisisitiza nafasi ya Cunningham, kwani si ajabu kwamba Pistons waligeuka kuwa timu makini msimu huohuo ambao mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alichaguliwa katika kikosi cha All-Star. “Cade Cunningham amefanikiwa kuingia All-Star. Kwa hiyo tayari msimu uliopita walikuwa kipenzi cha wengi. Ilikuwa hadithi ya kushangaza ya kile walichokuwa wakifanya,” aliongeza.

Kwa sasa wana rekodi ya ushindi wa mechi 15 huku wakipoteza mbili, na Cunningham anacheza vizuri zaidi katika kiwango cha MVP, na pia eneo lao la ulinzi limeimarika. “Cade Cunningham atakuwapo katika mjadala wa MVP. Sijui nafasi zake za kushinda kutokana na kuwepo Jokic, Luka, Giannis, SGA na pia bado hatujamtaja Wemby,” Stein amesema.

MV 03

“Kwa hiyo kuingia tu katika tano bora ya MVP ni mafanikio makubwa kwa Cade Cunningham. Lakini Pistons wana rekodi bora zaidi Mashariki. Yeye ndiye mchezaji wao bora. Kama haya yanaendelea, kama Pistons watamaliza msimu wa kawaida wakiwa na rekodi bora Mashariki nadhani Cade atalazimika kuingia kwenye top five ya mjadala wa MVP kwa namna fulani.”

Haitakuwa haki kuyahusisha mafanikio ya Pistons kupitia Cunningham pekee, kwani mchango wa Jalen Duren ambaye baada ya kuchaguliwa drafti ya 2022 amekuwa muhimu kwa  misimu miwili iliyopita, akionekana kuwa bora katika ribaundi na ni tishio katika mipira ya juu (lobs), bila kusahau kwamba ni bora kwenye 'pick-and-roll' kwa Cunningham.

MV 04

Stein anasema: “Cade Cunningham hata alivyo mzuri hawezi kufanya haya peke yake. Jalen Duren amekuwa bora na wa ajabu. Ana sifa ya kupata mkataba wa nyongeza.”

“Hakupata nyongeza hiyo ya mkataba, ambayo inamaanisha atakuwa mchezaji huru mwenye vikwazo majira ya kiangazi yajayo baada ya kucheza katika kiwango cha All-Star.”


WANAOTAJWA WENGINE

Ukimuondoa Cunningham, mastaa wengine wanaotajwa katika moto wa kinyang'anyiro cha MVP ni pamoja na

Nikola Jokic (Denver Nuggets), Shai Gilgeous-Alexander (Oklahoma City Thunder), Giannis Antetokounmpo (Milwaukee Bucks),

Luka Doncic (Dallas Mavericks), Jayson Tatum (Boston Celtics), Victor Wembanyama (San Antonio Spurs), Tyrese Maxey (Philadelphia 76ers), Donovan Mitchell (Cleveland Cavaliers) na Jalen Brunson (New York Knicks).

MV 05

KWA NINI NI WENGI?

Ni vigumu kutabiri wazi nani anaweza kuibuka MVP, lakini si tu juu ya mtu mmoja, lakini inahusisha takwimu za mtu binafsi, mafanikio ya timu, mchango wa mchezaji kwenye ushindi wa timu na jinsi mchezaji anavyoonekana kuongoza timu. Hivyo, mara nyingi kuna wachezaji kadhaa wana hadhi ya MVP kuanzia mwanzo wa msimu.

Zaidi ya hayo, mchezaji anayekuwa mgombea mwaka huu anaweza kushushwa na majeraha na mwingine akainuka — hivyo chaguo la MVP hubadilika katika mazingira ya ajabu.

Kwa kuzingatia orodha ya sasa inayotajwa tajwa, mastaa 10 kati ya 11 walikuwapo msimu uliopita na ni wazi kwamba msimu huu mmoja anaweza kuibuka kinara. Hiyo inaonyesha ushindani mkali na kuonyesha kuwa hakuna mwenye umili wa nafasi hiyo wakati msimu wa kawaida (regular season) ukikaribia mwisho.