Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Wolves yasajili kina Gomes wanne

WOLVES Pict

Muktasari:

  • Klabu hiyo inayopambana na hali yake kwenye Ligi Kuu England sasa ina wachezaji wanne wanaoitwa Gomes baada ya kumnasa kwa mkopo staa wa England, Angel Gomes, kutoka Marseille ya Ufaransa katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili la Januari.

LONDON, ENGLAND: WATANGAZAJI na wachambuzi wa soka watalazimika kuwa makini sana kwenye mechi za Wolverhampton Wanderers baada ya klabu hiyo kumsajili mchezaji wa nne mwenye jina linalofanana na wengine waliopo kwenye kikosi hicho.

Klabu hiyo inayopambana na hali yake kwenye Ligi Kuu England sasa ina wachezaji wanne wanaoitwa Gomes baada ya kumnasa kwa mkopo staa wa England, Angel Gomes, kutoka Marseille ya Ufaransa katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili la Januari.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 sasa ataungana na Joao Gomes wa Brazil, winga wa Ureno Rodrigo Gomes, na beki wa kati Toti Gomes kutoka Guinea-Bissau.

Katika utambulisho wa Angel mapema wiki hii, Wolves iliandika hivi kwenye X: “Je, bado kuna nafasi ya Gomes mwingine?”

Shabiki mmoja alijibu: “Wolves wanahitaji Gomes wangapi lol.”

Shabiki wa klabu pinzani alitania: “Kazi ya Wolves ni kuandika tu ‘Gomes’ kwenye kisanduku cha kutafuta na kumnunua mchezaji wa kwanza anayeonekana.”

Kwa bahati nzuri, beki Toti Gomes kwa kawaida huvaa jezi yenye jina lake la kwanza mgongoni.

Kuwa na wachezaji wanne wenye jina moja la ukoo kunadhaniwa kuwa ni tukio la kwanza katika Ligi Kuu England.

Hata hivyo, Machi 1960, klabu ya Crewe Alexandra iliwahi kuchezesha wachezaji wanne wenye jina Jones; Keith, Dick, David na Mervyn katika mechi ya Daraja la Nne dhidi ya Workington kutoka Cumbria. Ripoti ya mechi hiyo kwenye gazeti la eneo hilo ilikuwa na kichwa cha habari: “Keeping up with the Joneses!” Msimu uliofuata, Crewe ilisajili Jones wa tano, Peter.

Lakini Wolves bado ina safari ndefu kufikia rekodi ya klabu ya soka ya kijijini ya Kroatia, NK Vrcevo Glavica, ambayo mwaka 2016 ilikuwa na wachezaji 21 wote wenye jina la ukoo Stevanja.