Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Raheem Sterling anukia Roma

Muktasari:

  • Mchezaji huyo anatarajiwa kuondoka katika dirisha hili la usajili la usajili la majira ya baridi baada ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza cha Chelsea jwa muda mrefu sasa.

TIMU kadhaa kutoka Italia ikiwemo Napoli na AS Roma zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya England, Raheem Sterling, 31.

Mchezaji huyo anatarajiwa kuondoka katika dirisha hili la usajili la usajili la majira ya baridi baada ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza cha Chelsea jwa muda mrefu sasa.

Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, mwandishi aliyebobea katika ishu za usajili Ulaya, uongozi wa Chelsea na wawakilishi wa Sterling wamekuwa wakikutana katika mazungumzo juu ya  kumwezesha mchezaji huyo kupata klabu mpya ya kuitumikia kwa sasa, ambapo anaweza akaondoka kwa mkopo au mkataba wa moja wa moja.

Sterling amekuwa hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Chelsea jambo linalomsukuma kutaka kuondokana na hali hiyo ili akapate timu itakayompa nafasi ya kukiwasha.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika ifikapo 2027 na tangu kuanza kwa msimu huu akiwa na matajiri hao wa Jiji la London, hajacheza hata mechi moja ya ushindani na kuna nyakati alikuwa akifanya mazoezi na vikosi vya timu za wachezaji wadogo.

Roma imekuwa ikitafuta mshambuliaji tangu mwaka jana na baada ya kuona Sterling anaweza kuuzwa imeamua kuwekeza nguvu kubwa kuhakikisha inamsajili.

Mabosi wa Roma wanataka kumsajili staa huyo kwa mkopo wa nusu msimu ambao utakuwa na kipengele cha kumnunua mazima mwisho wa msimu.


Lewis Dunk

BRIGHTON imekataa ombi la Nottingham Forest  kumnunua beki mkongwe na nahodha wa kikosi, Lewis Dunk, 34, katika dirisha hili la usajili.Kwa mujibu wa Sky Sports, uongozi wa Brighton haupo tayari kumuachia mchezaji huyo kutokana na mchango wake mkubwa, hususan katika kipindi ambacho klabu hiyo inapambana kuimarisha kikosi. Dunk, ambaye ni zao la akademi ya Brighton amedumu katika klabu hiyo kwa miaka 15. Mkataba wake unamalizika 2027.


Cole Palmer

CHELSEA imesisitiza kuwa haina mpango wa kumuachia kiungo mshambuliaji, Cole Palmer (23), licha ya uvumi unaoendelea kumhusisha na Manchester United. Inadaiwa mabosi wa Chelsea wanamwangalia Palmer kama mchezaji muhimu na tegemeo katika kikosi cha kwanza, hivyo hawataruhusu kuona akiondoka kujiunga na timu nyingine. Palmer ambaye amewahi kucheza Manchester City kabla ya kutua Chelsea, mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2033.


Axel Disasi

WEST HAM United inapambana kukamilisha usajili wa wachezaji wawili kwa mkopo katika dirisha hili kipa wa Tottenham Hotspur, Antonin Kinsky, 22, na beki wa Chelsea, Axel Disasi, 27. Kwa mujibu wa The Guardian, ili mikataba hiyo miwili ifanikiwe West Ham italazimika kumrudisha beki wa kimataifa wa Brazil, Igor Julio, 27, Brighton  ili ipate nafasi ya kuwaingiza wawili hao katika mfumo.


Andre Onana

WAKALA wa kipa wa Manchester United, Andre Onana, 29, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo  Trabzonspor ya Uturuki, amezungumzia uwezekano wa mchezaji huyo kurejea katika klabu yake ya zamani ya Italia, Inter Milan, mwisho wa msimu huu. Kwa mujibu wa Daily Mail, Inter inataka kumsajili ili kuboresha safu ya ulinzi ikiamini ataonyesha kiwango bora zaidi kuliko cha kipa wa sasa. Inter inasikilizia uamuzi ya Man United.


Ward-Prowse

BURNLEY ipo katika mazungumzo na West Ham United ili kumsajili kwa mkopo kiungo wa kati wa kimataifa wa England, James Ward-Prowse, 31, katika dirisha hili. Burnley inataka mchezaji mwenye uzoefu kwa ajili ya kuboresha kikosi cha kwanza na Prowse anaonekana kuwa rahisi kupatikana kwa sababu sio tegemeo  West Ham. Mkataba wa Ward-Prowse, unatarajiwa kumalizika 2027. Msimu huu amecheza mechi sita za michuano yote.


Lassine Sinayoko

WOLVES imeongeza jina la mshambuliaji wa Auxerre na timu ya taifa ya Mali, Lassine Sinayoko, 26, katika orodha ya wachezaji Inaowafuatilia katika dirisha hili la usajili. Kwa mujibu wa Football Insider, Wolves imevutiwa na kiwango alichoonyesha katika michuano ya Afcon 2025. Hata hivyo, Wolves inakabiliwa na ushindani kutoka Coventry City na Middlesbrough.


Angel Gomes

WOLVES ipo katika mazungumzo na Marseille ili kumsajili kwa mkopo kiungo wa kati wa timu hiyo na England, Angel Gomes, 25. Kwa mujibu wa Talksport, Wolves wanamtazama Gomes kama mchezaji mwenye uwezo wa kuongeza ubunifu hasa kutokana na uwezo wake wa kuchezesha timu. Gomes, aliyewahi kupita katika akademi ya Manchester United, anapambania namba Marseille.